Je ungependa kumtuzia nini ili ajihisi kama unampenda? Kama bado haujafikiria, tumekundalia baadhi ya zawadi ambayo unaweza kumtuza umpendae:
Zawadi za rafiki wa kike:
Chokoleti
Hakuna msichana asiyependa vitu vitamu vitamu kama chokoleti. Ni vyema kununua box ya chokoleti na ikisindikizwa na maua mekundu.
Kuna vinwaji vya aina tofauti tofauti unayoweza kumpatia umpendae, na siku hizi unaweza kuandika ujumbe wa pekee kwa umpendae.
Vidani
Vidani vipo vya aina tofafauti bangili,hereni, pete na kadhalika, Waschana wanafurahia sana zawadi kama hizi. Hata kama itakua ni fedha au dhahabu, zawadi ni zawadi.
Zawadi za rafiki wa kiume:
Mavazi
Wanaume wana stahili kupendwa, cha kwanza mjue mwanaume wako je ni kitu gani haswa anapendelea katika mavazi kama ni suruali, tsheti, mashati, nguo na kadhalika. Ukisha jua hilo basi nenda dukani uangaze macho umpatie yule umpendae kitu kizuri.
Marashi
Chagua marashi iliyo ambatana na yeye jinsi alivyo. Kama unajua marashi anayopenda, itapendeza zaidi na ni uhakika kwamba atakufikiria kila anapoitumia.
Je kuna zawadi ambayo tumesahau?
Soma habari zingine hapa.
