Tunapoelekea katiks shamrashamra za siku ya Baba duniani, ni wakati mzuri wa kuonyesha upendo na kushukuru baba zetu kwa mengi waliyotofanyia , na jukumu lake kubwa katika familia. Kwa msaada kutoka kwa wahusika wa Maisha Magic Bongo, tumekusanya orodha za zawadi ambazo unaweza kumpa baba yako.
Kofia 🤠 (Nguzo – Mpali)
Umri ukizidi na nywele zinazidi kupungua kwa wanaume wengi. Chagua kofia kama ya Nguzo ndani ya tamthilia ya #MMBMpali kwa ajili ya baba yako.
Kompyuta Ndogo 💻 (Thomas – Jua Kali)
Kwa baba ambaye anapenda teknolojia, zawadi ya kompyuta ndogo itakuwa nzuri. Kwa mtu kama Thomas wa #MMBJuaKali anavyotuonyesha matumizi husika na kifaa hichi.
Kitabu 📚 (Chifu Pingu - Mwali)
Wengi wetu tunapenda kusoma, na baba zetu pia! Kwa sasa hivi Chifu Pingu wa #MMBMwali anaumwa na muda mwingi yupo ndani na kupitisha muda anasoma kidogo. Kwa baba yako unaweza kuchagua kitabu kinachofaa.
Vifaa vya Michezo 💪 (Roy – Huba)
Baba kama Roy amabaye bado ni kijana anapenda michezo, zawadi kama jezi ya timu anayoipenda, mpira, au kifaa cha kuchezea mchezo atakifurahia.
Je ni zawadi gani unaipenda zaidi? Tuambie hapo chini 👇Pia tunapenda kuwatakia baba zetu wote kheri ya siku hi maalum kwao.