Logo

Yajayo Mei Hii – Maisha Magic Bongo

Habari
01 Mei 2024
Pata ratiba yako ya vipindi vya Maisha Magic Bongo ndani ya mwezi huu!
Article

Jiya  – Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku

Katika Jiya, tunapata kufuatilia maisha ya familia iliyoundwa na tamaduni tofauti tatu, ambapo tofauti zao ndizo zinazowafanya kila mmoja kuwa wa kipekee. Mapenzi yanaposhinda hata mipaka ya tamaduni, rangi, na imani, huo ndio wakati inathibitisha tena kwamba upendo unashinda yote. Jiya, mwanamke Mhindu anayetaka kuolewa kwa lazima, anaamini kuwa amependa kijana mweusi Don G, lakini hatima ina mipango mingine wakati anapokutana na kijana Masaai Senteu na mambo yanageuka kabisa.

Kitimtim – Jumatatu na Jumanne saa 3 usiku

Ungana na Pili na familia yake ,hekaheka na maisha yao ya kila siku ni za kuvunja mbavu.

Mpali – Jumatatu hadi Alhamisi saa 2jioni

Sakata la Nguzo na wake zake zaidi ya sita ,maisha yao ya kila siku ni ya visa , visanga , mashindano , wivu , usaliti , kila mmoja akijaribu kuitetea nafasi yake. Jiunge na msimu mpya wa Mpali.

Huba – Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku

Jiunge na msimu mpya wa Huba na gundua matukio yatakao yokea ndani ya familia ya Mzee JB baada ya Tima kutoroka, Fei pia kutoroka nay eye kukabidhi kampuni yake kwa mkwe wake, Abby.

Jua Kali – Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku

Maria arudi na bado anamdanganya Frank kama mimba ni yake wakati akijua kwamba Thomas ndiye baba mtoto. Je ukweli utagundulika?

Wana wa Town – Jumapili saa 4 usiku

Kipindi hiki kina wafuatilia vijana wenye ushawishi, umaarufu, pesa na utanashati kwa mara ya kwanza wanatuonyesha maisha yao halisi, panda shuka zao za kazi, mapenzi, familia na mengine chungu nzima. 

Nuru (Marudio ya msimu wa kwanza) - Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku

Tamthilia hii inahusu ndugu wawili waliochukiana wanajikuta lazima waungane kupambana na adui anaewatandia giza nene maishani mwao, baba yao.

Mizani ya Ushambenga – Jumamosi saa 2:30 usiku

Malkia wa huba na Blandina , wanatupa vionjo vipya na mada za kusisimua zinazo husu maisha yetu ya kila siku.

Dosari  – Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku

Dosari inafuatilia maisha ya Queen, mwanamke aliye katika kivuli cha himaya ya mumewe na anayetafuta kisiri kulipiza kisasi kutokana na utoto wa kufadhaisha. Katika kipindi hiki, tunamuona akijaribu kupata mahali pake na utambulisho wake, wakati bado anatafuta upendo wa chaguo lake mwenyewe.

Jiunganishe na #MyDStv App kwa burudani zaidi.