Logo

Wazalishaji wa maudhui yetu hapa Maisha Magic Bongo

Habari
13 Juni 2020
Je, tunawajua wazalishaji wa vipindi tunavyopenda hapa Maisha magic Bongo?
Untitled design (3)

Kwa wiki mbili tunaungana na Wazalishaji na Direkta wakuu katika sekta ya burudani, Leah Richard na Aziz Mohamed.

Leah Richard, Mzalishaji na Direkta, Lamata Village Entertainment

Maudhui: Kapuni Season 1 – 3:

Leah aliingia kwenye sekta hii mwaka 2008. Amefanya kazi makampuni mengi kama steps entertainment kama director and scripty writer wa filamu 35, ikiwepo ‘Wake Up,in side’, ‘Gumzo’ na ‘Big Surprise’. Amefanya kazi Proin entertainment kwa kuzalisha filamu ikiwemo ‘Kigodoro na Figo’.

Leah amehusika na wasanii wa bongo fleva kama mwandiishi wa scripty za nyimbo na kusimamia video zao. Hawa wasanii kama Diamond Platinumz, Harmonize, na Weusi.

Kama mkurugenzi wa Lamata Village Entertainment, amewasimamia wasanii wa filamu za bongo.

“Nimefanya kazi za kutengeneza matangazo na makampuni mbalimbali ikiwemo Asas dairies Ltd na Star Times TZ. Vile vile, nimefanya kazi na DStv Tanzania kama producer wa tamthilia ya Kapuni kwa misimu mitatu toka kuanzia mwaka 2017 hadi 2020.

Leah ni mshindi wa tuzo ya ‘Malkia wa Nguvu’ mwaka 2019 katika kitengo cha burudani iliyotolewa na Clouds Media.

 

Aziz Mohamed, Mmiliki Mkuu, Big One Entertainment

Maudhui: Huba, Nyavu na Mizani ya Ushambenga

 Ndugu Aziz Mohamed Sharj ni miongoni mwa wahasisi wa sanaa za maigizo Tanzania.

Ni mtunzi,producer,direkta, muigizaji na mwandishi wa filamu na tamthilia mbali mbali.

Kwa sasa, ndiye Mzalishaji na Direkta wa vipindi, filamu na Tamthilia mbali mbali zinazo patikana ndani ya maisha Magic Bongo.

Tamthilia hizo ni Huba, Nyavu na vipindi vya ni kama Mchikicho wa Pwani na mwaka huu, akazingua kipindi cha Mizani ya Ushambenga.