Logo

Watu tuliowapoteza mwezi huu ndani ya Huba

Habari
28 Julai 2022
Mwezi huu ulikuwa na huzuni sana ndani ya Huba.
Untitled design (3)

Huu mwezi ulikuwa umejaa kilio ndani ya kipindi cha #MMBHuba. Baada ya Kashaulo kupoteza akili kidogo alijikuta na adui mkubwa. Wakati Annette na Miraj hawakuweza kusherekea mwanzo wa mahusiano yao baada ya Maisha yao kukatwa mapema.

Kashaulo

Kwa muda mrefu Kashaulo alikuwa akilinda siri ya Tesa baada ya kugundua kwamba Tesa ndiye aliyemuua mume wake, na baba wa Devi. Baada ya Sidi kumuacha, Kashaulo alichanganyikiwa kidogo. Hili jambo lilimfanya aanze kulopokalopoka vitu kwa watu. Baadhi ya vitu alivyokuwa anasema ni kwamba Tesa ni muuaji, kwasababu Tesa alikuwa anahofu kwamba atagundualiwa aliamua kumgonga Kashaulo na gari nah apo ndipo alifariki.

Annette

Baada ya kuachana na Carlos, Annette aliamua kwenda kufanya kazi kwa Tima. Wakati alivyokuwa kazini alikutana na Miraj na hapo ndipo walivyoanza mahusiano. Siku moja Miraj aliamua kumtoa Annette bahari na hapo ndipo Kibibi na Fabrizio walitokea na kumpiga risasi Miraj. Annette, alipewa boya la kuogelea na aliambiwa aogelee mpaka ufukweni, kwa bahati mbaya Annette alifia baharini.

Miraj

Kibibi alikuwa anajaribu kumuua Miraj kwa muda mrefu sasa. Baada ya baba yake Miraj, na mume wa Kibibi, kufariki alimuachia ulithi Kibibi na sio Miraj. Hili jambo lilimkasirisha sana Miraj na alijaribu kumuua Kibibi bila kufanikiwa na Kibibi alikimbia Zanzibar. Pale Kibibi alivyosikia kwamba Miraj alikuja Dar es Salaam, Kibibi alimtafuta na alifanikiwa kumumaliza.

Ni kifo cha nani kilikusikitisha zaidi? Tuambie hapo chini 👇👇

Untitled design (3)
Vifo ndani ya Huba

Ni kifo cha nani kilikusikitisha zaidi? Tuambie hapo chini

Kashaulo57%
Annette28%
Miraj15%