Logo

WASILISHA TAMTHILIA YAKO - MAISHA MAGIC BONGO

Habari
22 Agosti 2023
Tarehe ya kufunga 31/08/2023
Article

Maisha Magic Bongo ni moja kati ya chaneli bora zinazoenzi na kuburudisha kwa kutumia lugha ya Kiswahili ambayo inapatikana kwa watanzania wote kupitia huduma ya DStv Chaneli 160.

Chaneli hii huwa inatoa burudani kwa mambo mbalimbali ya jamii kwa kutumia lugha ya Kiswahili, ikiwa ni pamoja na filamu za Bongo Movies, Tamthilia, Mahojiano, vichekesho, maisha ya watu mbalimbali pamoja na muziki.

 

Maelezo kwa Muandaaji

Maisha Magic Bongo inapenda kutoa rai kwa watanzania ambao wanatengeneza tamthilia, kwamba tumeanza kupokea mapendekezo ya tamthilia. Tamthilia itakayo chukuliwa inatakiwa kulenga zaidi katika mazingira ya mila na desturi, mapenzi, mahusiano, vichekesho, na maisha ya watu mbalimbali.

Tamthilia inatakiwa kuandaliwa kwa lugha ya Kiswahili na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza (subtitle).

Tamthilia inatakiwa kuwavutia na kuwasisimua mashabiki ili wazidi kutaka kuiangalia tamthilia hiyo.

 

Mahitaji yanayopendekezwa

  • Kulenga watu wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
  • Muda-dakika 26
  • Lugha -Kiswahili
  • Mwongozo wa tamthilia (Synopsis)
  • Wasanii watakaocheza (Character Bible)
  • Majina kamili ya timu ya waandaaji
  • Bajeti ya Awali
  • Vielelezo vya kampuni, ikiwemo majina kamili ya kampuni, waongozaji na wadau, vielelezo vya usajili wa kampuni, hati za usajili za VAT na anuani kamili.
  • Demo ya mapendekezo/mfano wa kazi uliyoifanya. Inaweza kuwa ni tamthilia ama filamu.

               Tathmini

  1. Risiti za mapendekezo zitapokelewa kwa njia ya barua pepe.
  2. Mapendekezo yatapitiwa na jopo la majaji wa kitengo cha maudhui ya Mnet, ambao watatolea maelezo mafupi mapendekezo yaliyopitishwa.
  3. Kuchagua mapendekezo yaliyoshinda.

Viwango vya kitaalam na uhariri vinavyotakiwa na Maisha Magic Bongo vitawekwa kwenye mkataba wa makubaliano. Maisha Magic Bongo ndio watafanya uhariri wa mwisho na udhibiti wa ubunifu kulingana na matarajio ya kipindi kinachotakiwa.

Mwisho wa Ukusanyaji: 31/08/2023

Kila kitu kinatakiwa kutumwa kwenye Tovuti ifuatayo: -

Maisha Magic Bongo - M-Net Submissions (mnetcorporate.co.za)