Logo

Washindi ndani ya tuzo za Tanzanian Music Awards (TMA) – Kumi za Wiki

Habari
07 Mei 2023
Tanzania Music festival inayojuikana pia kama Kili Music Festival hufanyika nchini kila mwaka .
Article

Mwaka huu wasanii wengi wakongwe na wakizazi kipya walipata fursa ya kuingia na kutunukiwa tuzo mbali mbali miongoni mwa hao ni kama Zuchu aliyechukua tuzo kubwa 5 wengine ni , Diamond Platnumz, Bill Nass, Mbosso, Dulla Makabila , Rosa Ree na wengine wengi . 

Usiku wa Jumamosi ya tarehe 29 Aprilli 2023, ulikuwa wa shamrashamra katika tasnia ya muziki Tanzania baada ya kufanyika tuzo za muziki za Tanzania. Tuzo hizi hufanyika kila mwaka na huwakutanisha wanamuziki wote nchini Tanzania kushindania tuzo katika vipengele mbalimbali. Mwaka huu tuzo hizo zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katika usiku huo wa kipekee, kuliibuka washindi mbalimbali katika vipengele mbalimbali. Hii ndiyo orodha ya washindi wakubwa wiki iliyopita:
Mwanamuziki Bora wa Kiume – Harmonize
Mwanamuziki Bora wa Kike – Zuchu
Msanii Bora wa Kiume – Bill Nass
Msanii Bora wa Kike – Rosa Ree
Mwanamuziki Bora Chipukizi – Kontawa
Chaguo la watu (Kiume) – Diamond Platnumz
Chaguo la watu (Kike) – Zuchu
Produsa Bora wa Bongo Flava – Abbah 
Produsa Bora wa Hip Hop – S2KYZ
DJ Bora wa Kiume – Dj Ally B
DJ Bora wa Kike – Dj Mammie

Endelea kufuatilia miziki inayovuma ndani ya kipindi cha #MMBBass kila Jumatatu hadi Alhamisi saa 11 jioni na kipindi cha #MMBKumiZaWiki kila Ijumaa saa 11 jioni.