Logo

Wanandoa tuliowapenda mwaka huu  – #BestOf21

Habari
03 Decemba 2021
Maisha Magic Bongo ilitupa mifano mingi ya wanandoa tuliowapenda ndani ya huu mwaka.
Untitled design (21)

Ndoa sio rahisi na tuliona ndoa ambazo hazikuweza kufanikiwa mwaka huu ndani ya Maisha Magic Bongo, lakini pia tuliona ndoa ambazo ziliendelea vizuri ingawa hap ana pale kulikuwa na matatizo kidogo. Hapo chini kuna ndoa tatu tulizo zipenda sana mwaka huu:

Bidu na Tunu (Pazia)

Bidu na Tunu walianza vibaya, baada ya Bidu kumuokota barabarani Regina, Tunu alidhani kwamba Bidu alikuwa na michepuko ndani ya ndoa. Hili jambo lilimfanya Tunu awambie mapolisi kwamba Bidu ndiye aliyembaka Regina, hatimaye hukumu zote kwa Bidu zilifutwa baada ya Regina kuamka. Ukiachana na hilo jambo, shida zingine ziliyokea. Sikumoja baada kulewa Bidu alijikuta mikononi mwa Karembo. Baada yah apo Karembo aliamua kutumia nguvu ili amdhurumu pesa Bidu. Hiki kitendo kilimfanya Tunu aolewe na Sadic. Hatimaye baada ya kuona kwamba Bidu alimpenda sana Tunu, aliamua kurudiana nae na kwa bahati nzuri Bidu alikuwa mjamzito na alijifungua mtoto wa kike. Ingawa kuna wasiwasi na jinsi mtoto anavyofanana, Tun una Bidu wamerudi nyumbani na mtoto kama familia. Kumbuka kwamba #MMBPazia iko kwenye mapumziko mpaka mwezi wa nne mwakani.

Chidi na Happy (Huba)

Chidi na Happy walikutana wakati walivyokuwa wanawafanya kazi kwa Tima. Wakati Chidi alivyomuona Happy, alikuwa ndio amemaliza mahusiano na Kibibi. Kibibi na Chidi walizaa mtoto, Angel, na baada ya kuachana, Kibibi alimchukua Angel na kuhamia nae Zanzibar. Kitendo hiki kimfanya Chidi kuumia san ana kutoaminia wanawake. Lakini alivyokutana na Happy, alibadirika na walifunga ndoa kirasmi. Kwa sasa, Chidi na Happy wanampango wa kutoka nyumabni kwa Tim ana Jude ili waanzishe familia yao. Usikose kufuatilia ndoa ya Chidi na Happy kila Jumatatu hadi ijumaa saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.

Masantula na Da Zuu (Kitimtim)

Da Zu una Masantula sio wanandoa waki halali, ingawa wanaishi Pamoja, ndoa yao ni ya mkeka. Mwaka huu tumeona Da Zuu akitaka kubadirisha hilo jambon a anataka Masantula amlipie mahali harafu na kuvishwa pete. Tatizo limekuwa mwamba, Masantula hana pesa za kutosha za kufanya mipango yote. Hili jambo lilimkasirisha Da Zu una siku hizi, walianza kugombana sana. Kumbuka kufuatilia kama watafanikiwa kufunga ndoa ya halali kila Jumatatu na Jumanne saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.

Tuambie hapo chini kati ya hawa wanandoa ni nani alikufurahisha Zaidi mwaka huu?

Screenshot 2021 11 29 at 08
Tuzo la wanandoa tunaowapenda

Ni wanandoa gani kati ya hawa uliwapenda zaidi mwaka huu? Toa maoni yako hapo chini

Da Zuu na Masantula (Kitimtim)53%
Happy na Chidi (Huba)31%
Bidu na Tunu (Pazia)16%