Chanda – Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku
Azra anapigwa risasi, Yaz anapigana ili kuthibisha penzi lake kwake, uadui unainglia kati. Matukio ya kweli yaliyojaa upendo, chuki, kisasi na vifungo visivyoweza kuvunjika.
Kitimtim – Jumatatu na Jumanne saa 3 usiku
Ungana na Pili na familia yake ,hekaheka na maisha yao ya kila siku ni za kuvunja mbavu.
Mpali – Jumatatu hadi Alhamisi saa 12 jioni
Sakata la Nguzo na wake zake zaidi ya sita ,maisha yao ya kila siku ni ya visa , visanga , mashindano , wivu , usaliti , kila mmoja akijaribu kuitetea nafasi yake.
Huba – Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku
Huba likinyauka kwa Tima na Jude, mbolea ya kufa kuzikana ina nyunyuziwa katika bustani ya Nandy na Roy, Na ukweli mzima wa maisha ya JB unawekwa wazi.
Divas & Hustlas – Alhamisi saa 1 usiku (Msimu wa mwisho)
Wabunifu kwenye tasnia ya burudani wanapambana kukuza brand zao huku wakikumbwa na changamoto mbali mbali kwenye mishe mishe zao na maisha Yao binafsi.
Jua Kali – Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku
Meza zinageuka , Profesa Bill anavunja ukimya anayasema yote, na kila mwenye siri zote zinafichuka. Nani atabaki salama?
Wana wa Town Sunday saa 4 usiku
Kipindi hiki kina wafuatilia vijana wenye ushawishi, umaarufu, pesa na utanashati kwa mara ya kwanza wanatuonyesha maisha yao halisi, panda shuka zao za kazi, mapenzi, familia na mengine chungu nzima.
Nuru- Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku
Tamthilia hii inahusu ndugu wawili waliochukiana wanajikuta lazima waungane kupambana na adui anaewatandia giza nene maishani mwao, baba yao.
Mizani ya Ushambenga – Jumamosi saa 2:30 usiku
Malkia wa huba na Blandina , wanatupa vionjo vipya na mada za kusisimua zinazo husu maisha yetu ya kila siku.
Dhohari – Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku
Zahara binti wa KiZanzibari mwenye vipawa asivyovijua na kipaji cha kuimba, ndoto zake zinagonga mwamba mila na desturi zikihusika, mbaka pale anapokutana na Feisal na Sabina.
Jiunganishe na #MyDStv App kwa burudani zaidi.