Logo

Ukweli kuhusu baba yake Naira – Jua Kali

Habari
25 Agosti 2022
Profesa Bill agundulika kama ndiye baba yake na Naira
Screenshot 2022 08 25 at 14

Kwa muda mrefu Naira na mama yake, Auntie Zai wamekuwa wakiishi na familia ya Profesa Bill. Baada ya Auntie Zai kupata mimba, familia ya Prof. Bill ilimuonea huruma na walimpa kazi ya ndani na alimlea mwanae, Naira, ndani ya nyumba ya Prof Bill.

Nyumbani kwa Prof. Bill kuna watu wengi, mama yake Prof, mke wake, mtoto wake Bill Junior na ndugu zake Frank na Anna. Wakati mtoto wake Zai, Naira alivyokua, Frank alimtamani na alianza mahusiano ya kimapenzi nae kwa siri.

Wakati huu wote, Bill Jnr alianza kumpenda Naira pia. Alijaribu kumuomba Naira awe mpenzi wake lakini Naira alikataa juu ya kuwa anampenda Frank. Kwa bahati mbaya Naira aligundua kwamba amebeba mimba ya Frank na hakuweza kusema. Baada ya Prof. Bill kugundua kwamba mtoto wake Bill akuwa anampenda Naira aliamua kumwambia mama yake ukweli kwamba. Naira ni mwanae, na kwamba alimpa ujauzito mama Naira alivyokuwa ameoa mke wake na baada ya Zai kuzaa aliamua kumleta nyumbani kama mfanya kazi wa nyumba ili aweze kumlea Naira bila familia yake kugundua.

Sasa hivi Prof. Bill anataka kumwabia Naira ukweli, je Naira atamkubali kama baba yake?

Endelea kufuatilia Jua Kali kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku nfani ya #MaishaMagicBongo