Logo

Ukusanyaji wa Maudhui 2016: MMBongo Original Films.

Habari
26 Aprili 2016
Maisha Magic Bongo ingependa kutengeneza filamu halisi za kitanzania zinazolenga mila na desturi za kitanzania.
Ukusanyaji wa Maudhui 2016: MMBongo Original Films. Image : 20

MAUDHUI YA CHANELI
Maisha Magic Bongo ni moja kati ya chaneli bora zinazoenzi na kuburudisha kwa kutumia lugha ya Kiswahili ambayo inapatikana kwa watanzania wote kupitia huduma ya DStv Chaneli 160.
Chaneli hii huwa inatoa burudani kwa mambo mbalimbali ya jamii kwa kutumia lugha ya Kiswahili, ikiwa ni pamoja na filamu za Bongo Movies, Mahojiano, filamu za kihindi, vichekesho, maisha ya watu mbalimbali pamoja na muziki.

MAUDHUI YA MUANDAAJI:
AINA -Maisha Magic Bongo- Bongo Movie

MUDA - Filamu za dakika 90

MAELEZOMaisha Magic Bongo ingependa kutengeneza filamu halisi za kitanzania zinazolenga mila na desturi za kitanzania, mapenzi, mahusiano, afya na maisha ya watu mbalimbali. Filamu inatakiwa kuwa katika lugha ya Kiswahili na kutafsiriwa kwa lugha ya kiingereza (subtitle).

Simulizi inatakiwa kuwa yakusisimua na kumfanya mtazamaji kusubiri kwa shauku filamu zingine.

MAHITAJI YANAYOPENDEKEZWA:
• Kulenga watu wenye umri kati ya miaka 20 na 45
• Lugha -Kiswahili
• Mwongozo wa tamthilia
• Wasanii watakaocheza
• Majina kamili ya timu ya waandaaji
• Bajeti ya Awali
• Maelezo ya mkataba, ikielezea majina kamili ya kampuni, waongozaji na wadau, vielelezo vya usajili wa kampuni, hati za usajili za VAT na anuani kamili.
TATHMINI:
1. Risiti za mapendekezo zitatambulika kwa njia ya barua pepe.
2. Mapendekezo yatapitiwa na jopo la majaji watakaochaguliwa na Wakuu wa Chaneli ambao watatolea maelezo mafupi mapendekezo yaliyopitishwa.
3. Kuchagua mapendekezo yaliyoshinda.

JINSI YA KUKUSANYA:
• Ukusanyaji wa mapendekezo ya (HD files) utafanyika hadi 19 /02 /2016 kwenye flash katika anwani ya kampuni yetu:

Maisha Magic Bongo,MNET Offices, 2nd Floor, Local Productions Studio, Jamhuri Grounds off Ngong Road, Nairobi , Kenya.

• Njia ya upokeaji: HD files katika flash

 

Mwisho wa Ukusanyaji: 19/02/2016

• Viwango vya kitaalam na uhariri vinavyotakiwa na Maisha Magic Bongo vitawekwa kwenye mkataba wa makubaliano.
• Maisha Magic Bongo ndio watafanya uhariri wa mwisho na udhibiti wa ubunifu kulingana na matarajio ya kipindi kinachotakiwa.
Kila kitu kinatakiwa kutumwa katika anuani yetu ya ofisi:
Maisha Magic Bongo
MNET Offices,2nd Floor, Local Productions Studio
Jamhuri Grounds off NgongRoad, Nairobi, Kenya
Wasiliana na: Barbara Kambogi