maisha magic bongo logo

Tuzo za Tamthilia Tanzania zimefika Nyumbani

Habari
19 Decemba 2024
Tuzo za Tamthilia Tanzania kwa mara ya kwanza limefika Nyumbani , Tanzania kwa lengo la kutambua na kueneza mchango wa wadau, jitihada zilizofanywa na wasanii na mnyororo wa wahusika wote katika kufanikisha tamthilia
MMB_tuzozatamthilia_article_image_2024

Maisha magic bongo inakula shavu jingine tena kupitia tamthilia zetu na raundi hii mpaka walengwa wa nyuma ya kamera wanapaa kupitia jukwaa la Tuzo za Tamthilia Tanzania.


Waloteuliwa ndo hawa :
Wasanii uwapendao katika tamthilia ya JIYA, HUBA, KITIMTIM, DOSARI, GHARIKA na MPALI wameteuliwa kuania Tuzo za Tamthilia Tanzania mwaka 2024/2025, katika vipengele tofauti tofauti


Na hii ndio orodha ya baadhi ya wale walioteuliwa:


Muigizaji Bora Mwanaume (Best Actor)
Senteu (Gabo) – Jiya
Felix (Dennis Louis) – Jua Kali
Roy (Tito Zimbwe) – Huba


Muigizaji Bora Mwanamke (Best Actress)
Anna (Godliver Gordian) – Jua Kali
Nelly (Nelly Kamwelu) – Huba


Muigizaji Bora Mpambe Mwanamke (Best Supporting Actress)
Marji (Nusrat Rafique) – Jiya
Vivian (Lulu Diva) – Jua Kali
Tima (Asha Salum) - Huba


Muigizaji Bora Mpambe Mwanaume (Best Supporting Actor)
Jude (Benedict Kinyaiya) – Huba
Thomas (Stanley Msungu) – Jua Kali
Don G (Luckey Luckamo) – Jiya


Mwongozi mwema (Best Director)
Aziz Mohammed – Jiya
Aziz Mohammed – Huba
Leah Mwendamseke (Lamata) – Jua Kali


Picha Bora (Best Cinematography)
Abner Ondiek Anyang’ – Jua Kali
Tadeo G. David – Jiya
Godfrey E. Mtamani – Huba


Muswada Bora (Best Screenplay)
Zara Mwangi – Huba
Lea Mwendamseke (Lamata) – Jua Kali
Zaria Mohammed – Jiya


Muziki Bora (Best Music Score)
Switch Music Group – Jua Kali
Akili Mohammed – Jiya
Mbande Kinyo, Tacktick Music and Ngatale Music – Huba


Zoezi rasmi la kupiga kura limefunguliwa. Ili kupiga kura na kuona orodha kamili ya wale walio teuliwa:

  • Tembelea tovuti rasmi ya tuzozatamthilia.info
  • Katika ukurasa wa mwanzo, bofya kitufe cha VOTE
  • Chagua category unayopenda katika orodha na uchague jina na msanii aliyeteuliwa
  • Bonyeza msanii unaye muunga mkono katika ukurasa wa msanii ya ubofye VOTE
  • Ingiza idadi ya kura unayo taka kupiga na nambari yako ya simu na ubonyeze OK
  • Utapokea ujumbe wa SMS na pini ya udhibitisho. Weka pini hiyo ili kukamilisha mchakato wa kupiga kura
  • Kura moja ina thamani ya 1000 tsh

Unakaribishwa kupiga kura mara nyingi uwezavyo ili ukuze sanaa ya tamthilia za Tanzania.

Ahsante Sana!!!!