Logo

Tausi, Bikira Kidawa, Alhamisi, ndani ya MMBongo!

Habari
26 Aprili 2016
Filamu moto moto kila siku hapa Maisha Magic Bongo! Ni Yetu!
Tausi, Bikira Kidawa, Alhamisi, ndani ya MMBongo! Image : 15

MAUTI
ALHAMISI, 3 MACHI 2016


Mauti2


Luis ana ukoo wa familia iliyo na mali. Anakata shauri kumsaidia rafiki yake Peter ambaye Mamake mzazi ameugua. Mamake Luis, aiitwaye Masese anapata kiboko la penzi, na ampendaye? Lo! Anamtamani Peter! Masese anamshawishi na tunu na zawadi. Luis anakufa moyo na kukasirika kabisa. Anahamia kwa Mjomba wake mashambani. Muda unapita na Luis anaugua. Masese anakataa kutuma hela za matibabu yake. Pata mwisho wa mambo leo, hapa Maisha Magic Bongo!

BIKIRA KIDAWA
ALHAMISI
SAA 17:00 MPAKA SAA 19:00


Bikira Kidawa2.jpg

Dilunga ni Mpenda-Tembo. Mlevi chakari. Mke wake anachoshwa na tabia zake, kisha anampata mpenzi mwingine, Kombo.
Dilunga akamtoa kwa boma na kuwachwa na binti wake wawili, Siwema na Kidawa. Watoto hawa wakateseka kwa Baba yao kisha Siwema akatoroka mjini kutafuta riziki yake. Kidawa akawachwa nyumbani kuwatunza baba na Nyanya yao. Punde si punde, Diluinga akamposa Kidawa kuolewa ili apate mahari. Tazama mapambano katika maisha ya hawa wanawake watatu leo saa 17:00 EAT.


Wasiliana nasi katika kurasa zetu za facebook, Twitter na WeChat.