Logo

Safari ya ndoa ya Fibian na Getrude

Habari
26 Septemba 2019
fibian7

Fibian na Getrude Walikutana katika mazingira ya mihangaiko.Fibian alipomuona Getrude akamuomba nambari ya simu ili wahafamiane vizuri. Je mbinu gani ambazo Fibian alitumia kumsawishi Getrude hadi wakafunga ndoa?

Gallery

Mahusiano yao ya urafiki iliongezeka pindi Fabian alipogundua kuwa Getrude alikuwa Nesi na angeweza kumsaidia na maduka yake ya dawa anayeyamiliki. Wakati huo huo, Fabian alikuwa akichunguza kuona kama Getrude angeweza kuwa chaguo sahihi kwake. 

Fabian alikuwa na mtoto kutoka kwenye uhusiano wake wa zamani na, alikuwa akimtafuta mwanamke mwenye roho ya pekee ya kumjali na kumsaidia kumlea mtoto wake, katika misingi mizuri ya kimaisha.

Wakati Fabian alipomridhia Getrude, ndipo alipomuomba kuwa mke wake ndoa, Getrude hakusita kukubali ombi lake. Jamaa, marafiki na familia zao wanafurahi na wanaunga mkono kwenye uamuzi waliouchagua. Wapendao hawa wawili wanafunga ndoa huku wakitegemea kupata mtoto hivi karibuni. 

 

                                                                         Tukutane kila Alhamisi saa 1 Usiku na kupitia DStv 160