Logo

Sababu tano za kuangalia ‘Single Kiasi’ ndani ya Showmax

Habari
25 Januari 2022
Usikose vipindi vipya kila Alhamisi!
SINGLE KIASI SM 750x375

Kipindi cha Single Kiasi ni kipindi cha asili cha Kiswahili ndani ya Showmax baada ya kipindi cha Crime and Justice mwaka jana. Kipindi hiki kinahusu marafiki watatu, Sintamei, Mariah na Rebecca. Kipindi hiki kinafuatilia maisha yao na ndoa zao kwa ukaribu wakati wakiendelea kuwa marafiki jijini Nairobi. Kama bado haujakiangali, tutakupa sababu nzuri tano za kuangalia kipindi hiki:

     1. Kilichukuliwa toka kwenye ‘Unmarried’

Kipindi cha Unmarried kilukuwa kipindi maarufu sana nchini Afrika Kusini, umaarufu wake ulifika Afrika nzima lakini lugha ndiyo aliyokuwa tatizo kubwa. Single Kiasi tofauti na Unmarried ni ya Kiswahili, maana yake mtu yoyote ndani ya Tanzania na Kenya anaweza kufuatilia na kuelewa kuliko kipindi cha ‘Unmarried’.

  1. Gathoni Mutua

Gathoni anaigiza kama Sintamei kwenye kipindi cha Single Kiasi. Unamjua kutoka kwenye kipindi kilichopita cha Crime and Justice. Sintamei ni mwenye sheria anataka kupanda cheo kabla ya kukugundua mume wake alikuwa anatembea na mwanamke mwingine.

  1. Minne Kariuki

Unaweza kuwa unamjua Minne kutoka kwenye kipindi cha Ma’Empress, ndani ya Single Kiasi Minne anaogiza kama Maria, dada mzuri anayependa Maisha ya kifahari. Maria atafanya lolote kuonyesha kwamba anaishi Maisha ya kijuu zaidi.

  1. Faith Kibathi

Faith anaigiza kama mama wa nyumbani, Rebecca. Rebecca ana watoto wawili na aliolewa na mchumba wa kutokea shule ya sekondari.

  1. Inaelewesha jinsi watu wanavyochumbiana Nairobi.

Single Kiasi inaonyesha jinsi gani waswahili waishi na kuchumbiana ndani ya jiji la Nairobi. Kama haujawahi kufika, kipindi hiki kitakuonyesha kidogo ni jinsi gani madada hawa wanaishi na Maisha yao sio mbali san ana Maisha ya Dar es Salaam.

Kumbuka kuangalia vipindi vipya kila Alhamisi ndani ya Showmax!