Logo
channel logo dark

Mizani Ya Ushambenga

160Uhalisia13

PATA KUMJUA 'MALKIA WA HUBA' MWANTUMU HAMZA JUMA

Habari
22 Aprili 2022
'Malkia wa Huba' ajiunga na Mizani Ya Ushambenga ndani ya Maisha Magic Bongo
Screenshot 2022 04 07 at 15

Mwantumu Hamza Juma anajulikaa kama ‘Malkia wa Huba’. Alilelewa na na mzazi mmoja pamoja na wadogo zake watatu. Alikulia ndani ya Kijiji kidogo pamoja na bibi na babu yake. Maisha yake magumu yalimsahidia kuamua ni nini alitaka kufanya na maisha yake mpaka kuanza kuitwa “Malikia wa Huba”.

Alivyokuwa mtoto, alijikuta mpweke kasababu hakuweza kuelewana na watoto wenzake. Walezi wa Mwantumu walijaribu kumuhimiza Mwantumu ajiunge na hobi na shughuli za kitamaduni. Kuanzia hapo alijifunza Zaidi kuhusu desturi za Kiswahili. Wazee wa Tanga ni waliomuwezesha Zaidi kujifunza, ndani ya kikundi cha wakina mama cha Kiswahili kinachoitwa, Kungwi. Pale alijifunza kupika, kujipa heshima kama mwanamke, jinsi ya kuwa na wanaume na jinsi ya kuwa mwanamke wa Kiswahili.

Kuhusu kazi yake:

Kwenye upane wa kazi, Mwantumu alitokea mbali. Alianzia kazi ndani ya kikundi cha jamii cha sensa mwaka 2011 mpaka 2012. Kutoka hapo alipata kazi yake ya kwanza ndani ya radio kwenye stesheni ya TK ya Tanga ndani ya kipindi cha muziki wa Taarab, ndani ya mwaka 2019 mpaka 2020. Kutoka hapo aliajiriwa na kipindi cha television cha ‘Thinkers’ ndani ya kipindi cha maongezi cha ‘Utamu wa Pwani’ ambacho kilirushwa kwenye mtandao ya jamii mwaka 2021. Mwantumu ana uzoefu wa miaka minne kwenye vipindi vya maongezaji. Pamoja na hayo, ni mwana mitindi, mc na mshawishi wa chapa tofauti. Anapenda kusikiliza muziki, kupika na kusafiri.

Usikose kumuangalia Mwantumu ndani ya kipindi cha Mizani ya Ushambenga kila Jumamosi saa 2 usiku!