Logo
channel logo dark

Mizani Ya Ushambenga

160Uhalisia13

PATA KUMJUA BLANDINA ERNEST LUKINDO

Habari
15 Aprili 2022
Blandina ajiunga na Mizani Ya Ushambenga ndani ya Maisha Magic Bongo
Screenshot 2022 04 07 at 15

Blandina Ennest Lukindo, miaka 39, alikulia jijini Tanga na alisomea shule ya msingi na secondary hapohapo Tanga. Baada ya kumaliza shule, alihamia Uganda kusomea chou kikuu na alihitimu na shahada ya Wingi wa Mawasiliano.Blandina alizaliwa ndani familia ilikuwa na Watoto wanne, pamoja na wazazi wake alilelewa kwenye familia iliyo mleza kwa mil ana desturi za Kiswahili.

Kuhusu kazi yake: 

Anahudia vyombo vikuu vya Habari, mashirika yasiyo ya faida na vikao vya jamii, Zaidi ya jukumu lake la kuwa mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo. Pamoja na hayo yote, Blandina anauwezo wa kushawishi watu wengi chini ya mchambuzi wa huduma za jamii na tabia za watu. Haya yote ni kwasababu maoni yake yanathaminiwa sana, na watu wanaheshimu uamuzi wake. Blandina amejulikana sana ndani ya vituo mbalimabali vya redio na televisheni jijini Tanga kwa mfano; Mwambao FM ambapo alikuwa akifanya kipindi cha Taarab kuanzia mwaka 2007 mpaka mwaka 2010; alifanya kipindi cha Taarab cha Breeze FM 2010-2013, na hatimaye pia alijiunga na kipindi cha Taarab cha TK FM kuanzia 2018-2019. Ndani ya upande wa televisheni, alihusika ndani ya kipindi cha Taarab cha Tanga Televisheni 2014-2020, harafu alifanya Thinkers Online Television 2020 na sasa hivi anahusika na kipindi cha maongezi cha Utanu wa Pwani.

Ana mada ya kutaka maendeleo wa ukuaji wa muziki wa Taarab na pia miziki yote ya Kiswahili, na Maisha ya kijamii chini ya kipindi chake cha mazungumzo.Kwa juu Blandina anaonekana kama amejizatiti kuhusu mambo ya kijamii, mila za Waswahili na mambo ya ndoa na kadhalika. Haya yote wamewezekana kwa sababu ya malezi aliyoyapata kwa wazee wake wa Kungwi, yaliyomfanya awe mwanamke wa sahii wa Kiswahili. Ukiachana na kazi yake kama mtangazaji wa vipindi vya mazungumzo, yeye ni balozi wa chapa, anayependa kuogelea, kusiliza muziki, kutunga hadithi, kupika na kusafiri.

Usikose kumuangalia Blandina ndani ya kipindi cha Mizani ya Ushambenga kila Jumamosi saa 2 usiku!