Amapiano ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za muziki kama vile Jazi, House, na kundi la vyombo vya muziki vya Kiafrika. Wakati muziki huu ulianza kupata umaarufu nchini Afrika Kusini, watu walikuwa wanachukulia kama muziki wa Afrika Kusini pekee, lakini kwa sasa umeanza kupata umaarufu nchi mbalimbali, ikiwemo Tanzania.
Kuna nyimbo kadhaa za Amapiano ambazo zimekuwa maarufu sana nchini Tanzania. Hapo chini kumekuwekea orodha ya nyimbo tano za Amapiano zilizovuma sana nchini Tanzania:
- ‘Mama Amina’ ya Marioo, Sho Madjozi, na Bontle Smith.
Ndani ya wimbo huu Marioo akuletea mwanamuziki maarufu alishawahi kuigiza kwenye kipindi chetu cha #MMBJuaKali, Sho Madjozi Pamoja na mwanamuziki mwenzake tokea Afrika Kusini, Bontle Smith.
- ‘Chawa’ ya Rayvanny, Ntosh Gazi, na Whozu.
Hii ni moja ya nyimbo uliotamba sana juu ya mdundo wake.
- ‘IYO’ ya Diamond Platnumz, Focalistic, Mapara A Jazz, na Ntosh Gazi.
Hii ni moja ya nyimbo zilizodithibitisha kwamba Amapiano imefika Tanzania baada ya wanamuziki wa tokea Afrika Kusini kuja kufanya video hii Tanzania.
- ‘Mang'Dakiwe (Remix)’ ya Dj Obza, Harmonize, na Leon Lee
Wimbo huu iliimbwa kwa lugha ya Afrika Kusini lakini Harmonize alijiunga na kuongeza Kiswahili kidogo.
- ‘Teacher’ ya Harmonize
Mwimbo huu ni mchanyiko wa Kiswahili na lugha yake Harmonize ya nyumbani na mdundo wa muziki wa Amapiano.
Amapiano ni moja ya muziki ambao umeleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki nchini Tanzania. Nyimbo hizi za Amapiano zina ladha ya kipekee na zimepokelewa vyema sana na mashabiki wa muziki nchini Tanzania. Usikose kufuatilia miziki inayovuma nchini kila Jumatatu hadi Alhamisi ndani ya kipindi cha #MMBBass saa 11 jioni na pia kila Ijumaa ndani ya kipindi cha #MMBKumiZaWiki kupitia DStv chaneli 160! Je muziki wa amapiano wa Tanzania unapita ule wa Afrika Kusini? Toa maoni yako hapo chini 👇