Logo

Novemba hii ndani ya Maisha Magic Bongo!

Habari
01 Novemba 2023
Matarajio ya mwezi huu ndani ya DStv chaneli 160!
Article

Chanda – Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku

Azra anapigwa risasi, Yaz anapigana ili kuthibisha penzi lake kwake, uadui unainglia kati. Matukio ya kweli yaliyojaa upendo, chuki, kisasi na vifungo visivyoweza kuvunjika.

 

Kitimtim – Jumatatu na Jumanne saa 3 usiku

Ungana na Pili na familia yake ,hekaheka na maisha yao ya kila siku ni za kuvunja mbavu.

 

Mpali – Jumatatu hadi Alhamisi saa 12 jioni

Sakata la Nguzo na wake zake zaidi ya sita ,maisha yao ya kila siku ni ya visa , visanga , mashindano , wivu , usaliti , kila mmoja akijaribu kuitetea nafasi yake.

 

Huba – Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku

Huba likinyauka kwa Tima na Jude, mbolea ya kufa kuzikana ina nyunyuziwa katika bustani ya Nandy na Roy, Na ukweli mzima wa maisha ya JB unawekwa wazi.

 

Divas & Hustlas – Alhamisi saa 1 usiku

Wabunifu kwenye tasnia ya burudani wanapambana kukuza brand zao huku wakikumbwa na changamoto mbali mbali kwenye mishe mishe zao na maisha Yao binafsi.

 

Jua Kali – Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku

Meza zinageuka , Profesa Bill anavunja ukimya anayasema yote, na kila mwenye siri zote zinafichuka. Nani atabaki salama?

 

Wimbi - Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku

Simulizi za maisha ya watu yalioyojaa mitafaruko, dhoruba na taharuki zilizosababishwa na tamaa, usaliti, wivu na mapenzi.

 

Mizani ya Ushambenga – Jumamosi saa 2:30 usiku

Malkia wa huba na Blandina , wanatupa vionjo vipya na mada za kusisimua zinazo husu maisha yetu ya kila siku.

 

Dhohari – Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku

Zahara binti wa KiZanzibari mwenye vipawa asivyovijua na kipaji cha kuimba, ndoto zake zinagonga mwamba mila na desturi zikihusika, mbaka pale anapokutana na Feisal na Sabina.

 

Jiunganishe na #MyDStv App kwa burudani zaidi.