Logo

MMBongo: Ni siku yetu ya kuzaliwa!

Habari
03 Novemba 2016
Endelea kutazama na kufurahia burudani! Maisha Magic Bongo! NiYetu!
MMBongo: Ni siku yetu ya kuzaliwa! Image : 72

Maisha Magic Bongo ni chaneli kati ya chaneli nyingi zilizoanzishwa na campuni ya televisheni ya M-Net tarehe 1 Novemba 201. Chaneli hii ilianzishwa kwa madhumuni ya kutoa burudani kutoka Tanzania
Pamoja na kukuza vipaji,kutambua juhudi za waigizaji, wazalishaji na wakurugenzi wa filamu na televisheni na kuwapatia fursa mbali mbali waigizaji na waandaji wa filamu na vipindi mbali mbali Tanzania.

Katika chaneli ya Maisha Magic Bongo tunaitambua na kuienzi lugha yetu ya Kiswahili, tumejizatiti kutoa burudani kwa lugha yetu tamu ya Kiswahili.
Hivyo basi tukisherehekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa chaneli yetu, tungependa kutanguliza shukurani zetu za dhati kwa watu wote waliokuwa nasi tangu kuanzishwa kwa chaneli hii. Juhudi zenu tunazitambua lakini wa muhimu zaidi ni watazamaji wetu wapendwa nyie ndio kila kitu kwetu na ni kweli kwamba bila nyie hatuwezi, maoni yenu ya kila siku ndio yanayotuwezesha kuwaletea burudani kila siku.
Endelea kutazama na kufurahia burudani kutoka Tanzania filamu, Tamthilia na vipindi mbali mbali kupitia DStv 160 Maisha Magic Bongo Kweli NiYetu!Wasiliana nasi katika kurasa zetu za facebook, Twitter na WeChat