Logo

Nani alipagawa zaidi na mapenzi? – Huba

Habari
08 Septemba 2022
Kati ya Doris, Devi, Nelly na Sada ni nani aliyekoma na huba zaidi?
Untitled design

Mapenzi yanaweza kumfanya mtu yoyote apagawe na wahusika ndani ya #MMBHuba hawakuwa tofauti. Soma hapo chini kujua kwa zaidi walifanya nini juu ya mapenzi.

Doris

Baada ya Roy kumuacha Doris juu ya Nandy, Doris alianza kutumia madawa ya mizimu kumurudisha Roy kwake. Baada ya Roy kufanikiwa kurudiana na Nandy, aliamua kukubali kuwa mke mwenza na Nandy. Kwa bahati mbaya Doris hakufanikiwa kubeba mimba kama mke mwenza wake, Nandy. Hili jambo lilimfanya ambadirishe Nandy kuwa mbuzi nab ado anatumia madawa kuwa na Roy.

Devi

Devi alijikuta amemuoa Kibibi baada ya kuachana na Tima, ingawa bado alikuwa anampenda Tima. Baada ya kupata ajali akiwa anaelekea kurudiana na Tima apoteza kumbukumbu zote na arudiana na Kibibi ambaye aanza kumtesa. Baada ya kumuokoa Tima toka kwa Jude, Devi ataka kuanza mapenzi na Tima tena lakini Tima anasiri yake na hataki kumsamehe Devi. Hili jambo lamfanya Devi kujaribu kujiua.

Nelly

Nelly alikutana na Devi baada ya Kibibi kumuajili kama daktari wa kumsahidia kutembea. Wakati walivyokuwa wakizidi kujuana walianza kupendana na Tesa alivyogundua kwamba alianza kupenda alizidi kumuhimiza Nelly awe nae. Hili jambo lilimfanya aanze kunywa pombe mpaka kuchanganikiwa na kupigana na Tima.

Sada

Sada alivyokutana na Fabrizio alifikiri kwamba yeye ni mwanaume wa ndoto zake. Kwa bahati mbaya hakujua ni kazi gani Fabrizio anafanya. Baada ya Fabrizio kukamatwa na kutiwa jela juu ya kifo cha Miraj na Annette, Sada agundua kwamba Kibibi ndiye alikuwa bosi wake na Fabrizio na ndiye yeye aliye waua Miraj na Annette. Sada ajaribu kumuokoa Fabrizio lakini Kibibi amuonya kwamba atamua na pia ataua familia yake. Kwa sasa hivi Kibibi aanzisha moto nyumbani kwa Sad ana kaka yake yakub hapatikani baada moto.

Je nani alipagawa na huba? Tuambie hapo chini

Untitled design
Kupagawa na Huba!

Kati ya hawa ni nani amepagawa zaidi na mapenzi? Tuambie hapo chini

Doris28%
Devi41%
Nelly18%
Sada13%

Usikose kuangalia #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku na marudio kila Jumamosi saa 10:30 jioni ndani ya Maisha Magic Bongo kwa kupitia DStv chaneli 160!