Logo
channel logo dark

Kumi Za Wiki

160Muziki13

Wanamuziki wakuangalia mwaka huu – Kumi za Wiki

Habari
03 Februari 2022
Orodha ya mwanamuzi watakao paa mwaka huu!
Wine List Ebay Billboard (2)

#MMBKumiZaWiki inakuletea wanamuziki wapya ndani ya muziki ya Bongo Flava kila wiki. Mwaka jana tulifanikiwa kukutambusha kwa wanamzuziki wapya wenye vipaji mbalimbali. Hapo chini kumekuandali orodha ya wanamziki tunaowapenda na ambao wanazidi kupaa mwaka huu.

  1. Rayvanny

Rayvanny alikuwa mafrika wa kwanza kufanya tamasha ndani ya tuzo la muziki ulaya pamoja na msanii maarufu wa Colombia anayeitwa Maluma na nyimbo yao, Tetema. Usikose kumuangalia Rayvanny mwaka huu tunahisi kwamba atazidi kupaa zaidi na nyimbo mpya.

  1. Rosa Ree

Rosa ndiye mwanamke pekee kwenye orodha hii, mwaka huu tuliona jinsi umaarufu wake ulivyozidi baada ya kuigiza ndani ya kipindi cha Sinia na baadae kimataifa baada ya kuwa kwenye kipindi maarufu cha 90 Day Fiance’. Usikose kumuangalia kila wiki ndani ya #MMBKumizaWiki na mwimbo wake

  1. Mattan

Mattan anajulikana kwa wimbo wake uliovuma sana mwaka jana unaoitwa, Somo. Ingawa ndio bado ananza na kwenye muziki, mitindo y ana sauti yake inamuweka juu kwenye orodha yetu.

  1. Platform TZ

Platform TZ ndio kwanza anaanza na muziki lakini mwimbo wake unaoitwa, Who. Muziki wa Platform TZ ni mchanganyo wa rhumba na muziki wa Bongo Flava.

  1. Kusah

Kusah anapendwa sana na nchini, kuanzia jinsi alivyokuwa mpole na uzuri wake. Mwimbo wake, I wish ulivuma sana mwaka jana na umaarufu wake utazidi kupaa mwaka jana.

Je unafikiri ni nani atavuma zaidi mwaka huu?

Mwanamuziki wakuangalia mwaka huu – Kumi za Wiki

Je unafikiri ni nani atavuma zaidi mwaka huu?

Rayvanny32%
Rosa Ree9%
Mattan36%
Platform TZ11%
Kusah12%

Usikose kuangalia #MMBKumiZaWiki kila Ijumaa saa 11 jioni ndani ya Maisha Magic Bongo chaneli 160!