Logo
MMB HubaSM V1 TwitterCover Generic HR
channel logo dark

Huba

160Tamthilia16

Moto wa burudani kuendelea kuwaka ndani ya Maisha Magic Bongo

Habari
25 Machi 2022
Jua kali na Huba zaingia msimu mpya
Untitled design (19)

Mambo ndani ya chaneli ya Maisha Magic Bongo yanazidi kupamba moto ambapo tamthilia pendwa za Jua Kali na Huba zinaingia kwenye msimu mpya ulionogoeshwa na kuboreshwa zaidi. Tamthilia kongwe ya Huba inayomaliza msimu wake wa 10 imejizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa wapenzi wa tamthilia hapa nchini na nje ya nchi na sasa ifikapo Aprili 1, inaingia msimu mpya wa 11 ambao ni moto wa kuotea mbali ambapo waigizaji mahiri kama Kibibi, Devi, Tesa, Tima, Roy, Kashauro na wengineo wamejipanga kikamilifu kuwapa watazamaji burudani ya karne katika msumu huu.

Patashika itakuwa pale moto utakapomuacha mkokaji na kumchoma muotaji kwenye awamu mpya ya tano ya tamthilia namba moja ya Jua Kakali, msimu utakaoanza kurindima kuanzia Aprili 1, 2022. Ili kukata kabisa kiu ya mashabiki wake, tamthilia hii kabambe sasa itaonekana kwa siku 5 kwa wiki kuanzia Jumatano hadi Jumapili. “Haya yote ni matokeo ya sisi kama chaneli kusikiliza maoni na matakwa ya wateja wetu. Sasa tunawaletea vitu vile wanavyovipenda kwahiyo ndani ya Maisha Magic Bongo ni burudani isiyo na kifani” amesema Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi. Barbara amesema kuwa chaneli hiyo imeendelea kuongeza wigo wa kuchukua kazi za kitanzania na limekuwa jukwaa muhimu kuwatangaza wasanii wa Tanzania na kazi zao ndani na nje ya nchi.

Ameahidi kuwa Maisha Magic Bongo itaendelea kuboresha burudani kwa kuleta vipinddi vipya kila mara vinavyoendana na mahitaji na matakwa ya wateja hivyo wapenzi wote wa burudani hususani tamthilia waendelee kukaa mkao wa kula kwani burudani inazidi kupakuliwa ndani ya Maisha Magic Bongo.

Ni kipindi gani unakipenda zaidi? Tuambie hapo chini👇

Huba na Jua Kali

Ni kipindi gani unakipenda zaidi? Tuambie hapo chini

Huba11%
Jua Kali38%
Zote mbili52%

Maisha Magic Bongo inayopatikana DStv Chaneli 160  inapatikana katika kifurushi cha DStv Bomba cha Sh. 21,000 tu kwa mwezi. Chaneli hii ni mahsusi kwa maudhui na vipindi vya kitanzania na inaonyesha filamu, tamthilia, muziki, vichekesho, na vipindi vingine kadha wa kadha kutoka Tanzania.

Kwa mengine zaidi: