Logo
channel logo dark

Slay Queen

160Drama16 V

Mapenzi ya Pembe Tatu ya Derick Kasongo

Habari
22 Julai 2020
Derick Kasongo amejikuta akitekwa kwenye mapenzi ya pembe tatu kati ya Mamy na Agnes. Ni nani atamchagua?
SQ Article

Mamy na Agnes ni watu wawili tofauti sana, na kama umefuatilia #SlayQueenTZ kwa muda mrefu utajua kwamba kila mmoja ni maalum sana kwa Derick. Tabia za wanawake hawa wawili ni tofauti sana, hapa tutakupa tabia za kila mwanamke ambazo zilimvutia Derick wakati tukisubiri kujua ni nani atamchagua.


Mamy
Mamy na Derick wamejuana tangu sekondari, ila kwa muda walipoteza mawasiliano. Kabla mapenzi yao kuanza walikua marafiki sana lakini mavutio yaliongezeka walipo onana wakiwa watu wazima. Mamy ni mwanamke anaejielewa sana, anapenda vitu vya hali ya juu na maisha mazuri. Hapendi mtu wa kumpotezea muda na ni mwana mitindo mizuri sana.


Agnes
Agnes na Derick wamekutana ukubwani, Agnes amependwa sana na familia ya Kasongo na wamemkubali kuwa mke wa Derick. Derick mwenyewe anajua utulivu wa Agnes na jinsi anahitaji mwanamke ambaye anaweza kumletea heshima. Agnes ndio huyo mwanamke kwake, lakini jicho lake Derick bado halijatulia.


Kujua ni nani atamchagua, endelea kufuatilia tamthilia ya Slay Queen hapa Maisha Magic Bongo DStv chaneli 160 Jumatano mpaka Ijumaa saa 3:30 usiku na marudio kila Jumamosi kuanzia saa 8 mchana, ndani ya Maisha Magic Bongo chaneli 160 pekee