Logo
Divas & Hustlas
channel logo dark

Divas And Hustlas

160Lifestyle16

Mambo matano usiyoyajua kuhusu muziki wa Singeli – Divas & Hustlas

Habari
22 Novemba 2023
Muziki wa Singeli unaendelea kuvuma nchini Tanzania!
Divas & Hustlas

 

Kinata MC anajivunia kuwa msanii wa kwanza kuimba Singeli kwa Kiswahili ndani ya kipindi kinachovuma cha Divas & Hustlas ndani ya Maisha Magic Bongo.

 

  1. Singeli ilianza Tandale

Muziki wa Singeli ulianzishwa katika eneo linaloitwa Mtogole, Tandale, katika wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  1. Singeli ni mchanganyiko wa mitindo mitatu ya muziki

Mtindo wa muziki huu ni muunganiko wa aina tatu za muziki. Singeli ni muziki wa ngoma pamoja na densi ambapo MC huimba juu ya muziki wa taarab unaochezwa kwa haraka.

  1. Singeli una asili ya Kizaramo

Wazaramo ni kabila la watu nchini Tanzania wanaotoka Dar Es Salaam na Pwani, na wengi wao wanakaa Tandale.

  1. Singeli ilianza na shughuli mbalimbali jijini Dar es Salaam

Muziki wa Singeli ulianza kuvuma mwanzoni mwa mwaka 2000 baada ya baadhi ya MCs kufanya shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuandaa vigodoro katika mitaa ya Manzese na Tandale, na walipenda kuwaalika wanawake kucheza.

  1. Mwanzilishi wa kwanza wa Singeli alikuwa Bwana Msaga Sumu

Msaga Sumu anajulikana kuwa mwanzilishi wa kwanza wa muziki wa Singeli pamoja na marafiki zake.

 

Je, unapenda kusikiliza Singeli? [poll]

 

Kwa burudani zaidi, usikose kuangalia kipindi cha #MMBDivasAndHuslas kila Alhamisi saa 1 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.