Logo
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Maisha Magic Bongo yashinda vipengele 9 ndani ya tuzo za Bodi ya Filamu Tanzania

Habari
23 Decemba 2021
Jua Kali na Kititim vya shinda kwenye Tuzo za  Bodi ya Filamu.
Screenshot 2021 12 23 at 18

Mwaka huu tuliona serekali ikituletea tuzo za kwanza za filamu kupitia Bodi ya Filamu nchini Tanzania (Tanzania Film Festival Awards). Tuzo hili lilifanyika tarehe 18 mwezi wa Decemba, jijini Mbeya likuhudhuliwa na mgeni rasmi, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Innocent Bashugwa. Maisha Magic Bongo iliteuliwa kwenye vipingele 16 vya waigizaji na vipindi, na kwa pamoja, tulisha vipengele 9 vifuatavyo:

 

KITIMTIM – tuzo moja

  1.  Tamthilia bora ya vichekesho

 

JUAKALI  - tuzo nane

 

  1. Director bora - LEAH MWENDAMSEKE
  2. Tamthilia bora - JUAKALI
  3. Muigizaji bora wa kike – GODLIVER GORDIAN (ANNA)
  4. Muigizaji bora wa kike kwa chaguo la watazamaji – MIMI MARS (MARIA)
  5. Mutungaji bora wa muziki ­­- JUAKALI
  6. Muigizaji bora wa kike anaye sahidia – HELLEN HERMA (LOVE)
  7. Muundo bora wa uzalishaji - JUAKALI
  8. Muigizaji bora wa kiume kwa chaguo la watazamaji – MOHAMEDY KINGARA (IDDY)

 

Tunapenda kuwapa hongera washindi wote, Maisha Magic Bongo inajivunia sana kuwa na vipaji hivi!