Logo

MAISHA MAGIC BONGO IMEFIKA!

Habari
26 Aprili 2016
MAISHA MAGIC BONGO IMEFIKA! Image : 30

MMBongologo1resized

 

MAISHA MAGIC BONGO IMEFIKA!
CHANELI MPYA INAYOZINDULIWA NA M-NET KUWALENGA WATANZANIA.


Kampuni inayoongoza kwa burudani barani Afrika, M-Net inazindua chaneli mpya yenye kulenga watanzania, itakayokuwa na burudani mbali mbali zenye hadhi ya Kitanzania, ni MAISHA MAGIC BONGO itakayoanza kuonekana hewani Oktoba 1 saa 10 Alasiri. Moja ya madhumuni ya M-Net ni kuhakikisha inalifikia soko la wateja wake ikiwemo kuingiza maudhui wanayopenda wateja wake. Chaneli hii mpya inategemea kukidhi mahitaji ya soko la wateja wa Tanzania.

Ikihusisha vipindi zaidi ya 6 vitakavyokuwa vikiruka kila siku, MAISHA MAGIC BONGO itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Afrika Mashariki kupitia chaneli 160. Mbali na kuonyesha filamu kali kutoka Bongo Muvi na tamthilia za Kiswahili zinazopendwa na kufatiliwa nchi nzima, chaneli hii pia itakuwa ikionyesha vipindi vya maisha ya wa Tanzania, Muziki ukiwemo Bongo Flava , Maisha ya Mastaa na vipindi vya majadiliano ya moja kwa moja , bila kusahau sinema kali za kihindi kutoka Bollywood zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Akizungumza juu ya uzinduzi wa 'MAISHA MAGIC BONGO, Mkurugenzi wa M-Net kwa Afrika Mashariki Theo Erasmus anasema, " Tumefurahi kufunua mkondo huu mpya na kwa kuendelea mbele tunatarajia chaneli hii itakuwa moja ya chaneli pendwa zaidi Tanzania kwa msaada wa watazamaji wetu wa Tanzania ambao daima wamekuwa waaminifu kwetu na ndio sababu M-Net leo tumeamua kuwaletea chaneli hii mahususi kwa ajili yao.
Tunashukuru zaidi tumeweza

kupata baadhi ya vipindi bora kutoka kwa wazalishaji wakubwa kutoka ndani ambao wanashirikiana nasi, pia tunaangalia namna ya kupanua ushirikiano wetu zaidi na wazalishaji hawa wa filamu na vipindi vya runinga ili kuhakikisha kwamba mafanikio yao yanakuwa makubwa zaidi.

Ni mwezi sasa, tangu DStv ilipotangaza kwenye maonyesho ya maudhui nchini Mauritius, MAISHA MAGIC BONGO ipo tayari kuzinduliwa, na baadhi ya vipindi vitakavyokuwemo kwenye chaneli hii ni:

• Filamu za kibongo zitaonyeshwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 17:00 jioni, pia Jumamosi na Jumapili saa 19:30 usiku. Wakati huo huo Filamu za kihindi zilizotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili zitakuwa zinaonyeshwa kila siku ya Ijumaa saa 19:30 usiku. Baadhi ya Bongo Muvi maarufu zilizopo kwenye ratiba sasa ni Hard Price, Jimmy, Nampenda Motika na Nusra, na baadhi ya za kihindi ni I am 24, Jimmy, Anwar na Amar Akbar Anthony.

• Upande wa Tamthilia , jiandae kupata Talaka ( Jumanne saa 19:00 usiku ), usikose Mtaro ( Jumatatu saa 19:00 usiku) Isiyopitwa na muda Siri ya Mtungi ( Jumamosi na Jumapili saa 18:00) na ya vijana zaidi Dunia Tambara Bovu ( Ijumaa saa 19:00 usiku). Wasanii wenye vipaji waliopo kwenye tamthilia hizi ni kama vile Hamis Korongo , Alafa Arobain , Paulo Francis, Juma Rajab Rashid, Hidaya Maeda, Daudi Michael, Caroline Hussein na Habibu Seif na wengine wengi, hakika hii si ya kukosa!

• Bila shaka, MAISHA MAGIC BONGO pia itakuletea vipindi viwili vya muziki, Mzooka (Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 Alasiri) itakupa burudani ya video mpya kali kutoka Bongo, wakati kipindi cha Sifa Mix kitakuwa kikikujia ( kila Jumapili saa 11:00 asubuhi) ikikuletea muziki laini wa nyimbo za Dini.

• Pia kuna vipindi majadiliano utaviona kwenye chaneli hii, kama vile Mkasi ( kila Jumapili saa 16:00 EAT ) ambazo inazungumzia maisha ya wasanii wakubwa Tanzania, kisha hakikisha hauachi kumfuatilia Mboni (Jumamosi saa 15:00 EAT) Mboni Masimba akifanya mahojiano na watu mashuhuri , wajasiriamali, viongozi wa jamii na siasa , kujadili mada mbalimbali kuanzia utamaduni wa kiuchumi.

• Pia kwenye MAISHA MAGIC BONGO, usikose kuangalia kipindi cha Ajabu, kinachoburudisha na wakati mwingine kuogopesha lakini muda wote kitakuburudisha (Jumatano saa 19:00 Usiku).

Hivi pamoja na vingine kibao ambavyo si vya kukosa kwenye chaneli hii mpya, hakikisha unaangalia MAISHA MAGIC BONGO kuanzia usiku wa leo! Tembelea tovuti www.maishamagic.tv kwa maelezo zaidi.