Logo

Mabadiriko mapya ndani ya chaneli Maisha Magic Movies!

Habari
03 Mei 2023
Mwezi wa Mei unakuletea mabaridiriko makubwa ndani ya chaneli zetu
Maisha Magic Bongo Articles

Kuanzia mwezi wa Mei nakuletea mabariko kidogo ndani ya Maisha Magic Movies. Habari na video zote zitapatikana ndani ya tovuti ya #MaishaMagicEast wakati mitandao ya jamii ya Maisha Magic Bongo itazidi kukuletea taarifa kuhusu filamu halisi za Kitanzania ili kusaidia kukuza filamu za Kitanzania. Usikose kuangalia filamu za kitanzania kila Jumatatu na Ijumaa ndani ya DStv chaneli 141.

Orodha ya filamu za wiki hii:
Tego (5 Mei, saa 8:10 mchana)
Baada ya ndoa yake kutofanikiwa, mwanamke aamua kumroga kijana ili akae nae.

Ndoto Kubwa (5 Mei, saa 9:45 mchana)
Kijana mwenye malengo makubwa, Arnold aungana na mcheza mpira mstaafu, Masembe kwa lengo la kutwaa ubingwa wa taifa.

Kuku Kienyeji Part 1 and 2(5 Mei, saa 11:10 jioni)
Akiwa katika safari ya kwenda nyumbani kwao kijijini, kijana mmoja akutana na msichana wa kijijini na aamua kumpenda na mapenzi yao yapata majaribu.

East Zuu (5 Mei, saa 1:30 usiku)
Baada ya kijana  kuhaidiwa kazi bora, anakusanya jamii yake katika juhudi za kutafuta pesa. Bila kujua, yeye ndiye anayelengwa na kundi la wahuni wanaouza nafasi za uwongo za ajira.

Endelea kufuatilia @maishagicbongo ndani ya Instagram, @maishamagictz ndani ya Twitter na pia Maisha Magic Bongo ndani ya Facebook  kujua ni filamu gani zita onyeshwa ndani ya Maisha Magic Movies.