Logo
channel logo dark

Sinia

160Tamthilia16

Leila ampiga risasi Rose – Sinia

Habari
24 Agosti 2021
Baada ya kuamka Rose akumbuka ni nani aliye mpiga risasi
Screenshot 2021 08 25 at 10

Rose ni mke wa Mr Venus, na Pamoja wamejenga Maisha mazuri na Maisha ya kifahari. Lakini kama ndoa nyingi, ndoa yao pia inasiri nyingi. Siri ambayo tunajifunza mapema ni kwamba Mr Venus ana mchepuko, Leila.

 

Kwa Leila, Mr Venus sio mpenzi wake pekee, ana mahusiano na Marcus na anampenda Marcus sana. Tatizo ni kwamba Marcus hana pesa na Pamoja na Leila waandaa mpango wa kumuua Rose ili Leila amuoe Mr Venus harafu akisha muoa amuue ili yeye na Marcus waishi Maisha ya kifahari na pesa za Mr Venus na Rose

 

Kwa bahati mbaya mpango wao wa kumuua Rose haukufanikiwa na baada ya kupigwa risasi Rose akumbuka yote yaliotoke. Rose akataa kusema ni nani aliye mpiga risasi wakati Mr Venus aambiwa na Melinda ni nani aliye mpiga Rose risasi.

 

Baada ya Mr Venus kugundua kwamba ni mchepuko wake aliye jaribu kumuua mke wake, je atafanya nini? Usikose kuangalia #MMBSinia kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku.