channel logo dark
Mengine Zaidi
channel logo dark

Pazia

160TamthiliaPG13

Kutana na Timu ya #KitimtimTZ

Habari21 Septemba 2020
Kitimtim ni kipindi cha vichesho kinachovuma sana Tanzania na kimefanikiwa sana mpaka kufika msimu wa 12.
Kitimtim Article Sept

 Msimu huu umeanza na kasheshe kali sana; kuna ujauzito upya na pia tumeona muuigizaji mmoja akitoka. Lakini vichekesho bado vinaendelea na hii ndio timu inayo tuacha mbavu zikiuma kila Jumatatu na Jumanne.
 Pili
Pili, ndiye dada mkuu anayechezwa na muigizaji, Gladness Kifaluka. Yeye ni mke wa pili wa Zunde, na misemo yake imekuwa ikituacha hoyi kila wiki tangu Kitimtim ilivyoanza. Siku hizi unaweza kumwonya Gladness akiigiza kwenye kipindi chetu kingine kinachovuma ndani Maisha Magic Bongo, #NyavuTZ akiwa anaigiza kama ‘Rosa'.


Zunde
Zunde anaigizwa na Bwana Tiny White, Zunde anajulikana kwa hasira zake na maamuzi yake ya haraka. Ana wake wawili, Pili and Tabu; lakini hivi karibuni aliamua kumpa Tabu talaka.

Masantula
Masantula anaigizwa na Elisha Kawia; Masantula anapendwa sana na watazamaji kwa jinsi alivyokuwa mtu wa vichesho sana lakini sio vichesho vya kulazimisha, na kwa hilo watu wengi wamemkubali.

Da Zuu
Da Zuu ni mtu watu wengi wanaweza kumuelezea kama machacha sana ndani ya Kitimtim; anaigizwa na Dull Van. Ingawa Da Zuu ni mwanamke wengi wanapenda Dull Van aliweza kuiza kama vile mwanamke. Da Zuu sasa hivi ni mjamzito na anajitahidi kuficha lakini, mkosi inazidi kumfuata na siri yake.
 
Usikose #KitimtimTZ kila Jumatatu na Jumanne ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.