Msimu wa tano wa #SlayQueenTZ umetuletea waigizaji wengi wapya kwenye tamthilia yetu. Tuli, anaonekana sana kwa sababu yupo yupo tuu lakini hamna mtu ambaye amesha weza kumuelewa – na hatujui amefuata nini au kama ametumwa.
Mara ya kwanza tulivyo kutana na Tuli, alikuwa anatokea kwenye hoteli moja na Hans. Yeye ndio alikuwa wa kwanza kabisa kumuona Hans, inaonekana kama alimsoma Hans kidogo. Akamuita na kuomba msaada wake. Hapo ndipo alipochukua nafasi hiyo kumubadirishia simu Hans na ya kwake. Alifanya hivyo, ili aweze kumlazimisha Hans amtafute yeye baadae.
Hans ndio amerudi Tanzania kutoka masomoni nje ya nchi. Amefanikiwa kupata kazi mpya na bado anampenda mchumba wake wa zamani. Huyo mchumba wake, ndiye aliye msahidia kutafuta simu yake kipindi alivyo badirishana na Tuli. Hans amejikuta akivurugiwa akili na Tuli lakini bado haja muamini. Anaanza kukolea na penzi lake kwa Tuli na kuanza kumsahau mpenzi wake wa zamani. Je Hans atafika sehemu na kugundua kwamba Tuli anamchezea, au safari kwake ndio imeishia kwa Slay Queen mpya, Tuli?
Usikose haya yote kwenye #SlayQueenTZ kila Jumatano mpaka Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.