Logo
channel logo dark

Kumi Za Wiki

160Muziki16

Jumanne Iddi na Baba Levo wanapepea katika chati ya Kumi za Wiki!

Habari
05 Juni 2020
Ngoma moto moto na video za Bongo Fleva zinatua nanga hapa katika Maisha Magic Bongo! Tulipata mda wa kuongea na wasanii mashuhuri waliofika kilele cha chati yetu wiki mbili zilizopita!
Screenshot 2020 06 09 at 12

Kama kawaida, tunaendelea kuzingua maudhui, vipindi vya kipekee na burudani halisi hapa Maisha Magic Bongo! Tungependa sana kuwakilisha mabingwa wa muziki wetu wa kiasili. Kipindi cha Kumi za Wiki kinaendelea kuwakilisha muziki wetu, na waTanzania wanailkubali kabisa!

Tulikuwa na wasanii wawili walioweza kuchukua nafasi ya kwanza katika chati ya KZW. Hii ni kumaanisha wako tayari kabisa kupokea muziki na burudani ya kisasa. Wasanii hawa wantupatia simulizi ya Maisha na safari yao katika sekta ya uimbaji na uzalishaji wa Muziki.

 

Mshindi wa KZW  

Jumanne Iddi – ‘Baba’

Jumanne alikuwa Kijijini na kumpoteza baba yake mzazi akiwa mtoto. Jambo hili lilimwacha na hofu sana. Huyu msanii chipukizi alianza kutamani utaalam wa usanii akiwa bado mchanga. Jumanne anaeleza uhamasishaji wa ngoma ya baba, “Ni ngoma nyingi sana zimeandikwa kwa ajili ya kuwashukuru na kuwaheshima akina mama. Ngoma yangu ni ombi la kipekee, nikimheshimu sana hayati baba yangu mzazi.” Jumanne anawashauri wasanii wanaochipuka katika sekta ya muziki “Jiamani na kiudhamini sana talanta yako. Usiipuuze.”

 

Mshindi wa KZW 

Baba Levo – ‘High na Low’

Baba Levo aliyetoka Kigoma ni msanii kikongwe katika mada ya hiphop kwa sekta ya muziki. Simulizi yake inasisimua kwa kweli. Levo aliwahi kufungwa gerezani mara mbili kwa muda wa miezi nane. Wakati huu, alianza uandishi wa ngoma yake “High na Low”. Ngoma hii imechukua muda wa mwaka mmoja kufikia mashabik. Wakati Levo alikuwa anajiandaa kuzindua show zake, dunia ilikumbwa na janga la Corona na mashughuli yote ya kijumuiya kukomeshwa kabisa. Baba Levo alikuwa na haya ya kusema: “Kama ningekomesha juhudi zangu za kuipromoti Ngoma hii wakati huu wa Corona, mashabik wangu hawangepata fursa ya kuisikiliza kwa makini. Ujumbe wangu ni wa msingi kwani ninagusia maswala ya ugaidi, ufisadi na unyanyasaji wa wananchi ni polisi. Serikali za Afrika zinatakiwa kubadilisha mitindo yao. Ukipewa ujumbe na Mungu, tumia kipawa chako kueneza ujumbu huu. Usiogope.”

Ni wasanii wagani wameshikilia nafasi za tano kwa hizi wiki mbili?

Namba 6:

Maua Sama – ‘Nioneshe’

 

Namba 5:

Baraka De Prince – ‘Nimekoma’

 

 

Namba 4:

Tommy Flavour ft.Alikiba – ‘Omukwamo’

 

Namba 3:

Zuchu – ‘Wana’

 

Namba 2:

IBRAH – ‘Nimekubali’

 

Ni yupi atakaye ongoza jeshi letu pendwa la WanaBongo fleva wiki hii? Kuna ngoma mpya zitaingia katika Top 5? Mashabik wataamua!

Tazama highlights hapa!

 

Endelea kuungana nasi kila Ijumaa saa 11.30 jioni hapa Maisha Magic Bongo kupiita DStv chaneli 160. Tungependa kupata ujumbe wenu katika kurasa zetu za kijamii, @maishamagicbongo