Logo
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Jua Kali wapata tuzo la kimataifa

Habari
16 Aprili 2021
Jua Kali ishinda tuzo la kimataifa la Zikomo nchini, Zambia.
Instagram Post 1080x1080

Zikomo Awards ni tuzo kubwa ndani ya nchini Zambia, inaangalia watu bingwa ndani ya sehemu ya burudani na sanaa kadhalika. Mwaka huu, Zikomo Awards zilizidisha tuzo zao ili kuweka Pamoja tuzo za wanamitindo, muziki na watu wote wanaofanya kazi za hisani ndani ya bara la Afrika.

Mwaka huu, Zikomo Awards zilikuwa ndani yam ji wa Lusaka, Zambia. Kulikuwa na makundi ya kuzidi ishirini ya uteuzi tofauti na kipindi kinachopendwa sana ndani ya Maisha Magic Bongo cha Jua Kali kilifanikiwa kuteuliwa. Na walifanikiwa kurudi Tanzania na tuzo mbili; Best TV Soapie in Afrika (Kipindi bora cha tamthilia ndani ya bara la Afrika) na pia walichukua tuzo linguine kwa Best Movie Director in Africa (Direkta bora ndani ya bara la Africa) kwa direkta wa #MMBJuaKali, Leah Lamata.

Jua Kali ni kipindi cha Maisha Magic Bongo kilichoanza kuonyeshwa ndani ya chaneli ya DSTV 160, Januari mwaka 2021. Kipindi hiki kinausu Professor Bili ambaye ni bingwa wa kupiga hesabu zake huku akiwatumia watu mbalimbali katika michezo yake michafu. Mpambe wake Thomas, moja ya wanafunzi wake vipanga. Direkta wa Jua Kali ni Leah Lamata amabaye anaye julikana kama mwandishi bingwa wa filamu na direkta bingwa nchini Tazania.

Tunapenda kuwapa hongera kundi nzima la #MMBJuaKali kwa kazi nzuri na tunajivunia kuwa na vipaji hivi ndani ya Tanzania. Endelea kuburudika na vipindi vya #MMBJuaKali kila Jumatano mpaka Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo,chaneli 160.