Joachim Marunda Msaafiri Kimaryo maarafu kama ‘Master J’ anatoka katika familia ya Watoto wawili , yeye akiwa wa kwanza na ana mdogo wa kike.
Kama mtayarishaji wa muziki hodari nchini Tanzania na mmiliki wa studio ya Muziki ya MJ Records, Master J amefanya kazi na kukuza vipaji vya wasanii wengi sana Tanzania.
Tangu mwaka wa 2007, Master J amekalia kiti cha mmoja wa majaji katika mashidano ya Bongo Star Search, ‘BSS’.
Kipindi hicho maarufu hakikuweza kutambulika peke yake bila ya Master J.
Kabla ya kukomaa kama producer mkuu nchini Tanzania, Master J amepitia mengi katika maisha yake binafsi na familia .
Master J akiwa mdogo ndoto yake kubwa ilikuwa kuwa rubani. Kutokana na utundu kupita kiasi Master J hakuwa anafanya vizuri darasani , mpaka pale walipo hamia Botswana.
Ndoto yake ili balilika wakati alikuwa huko huko shuleni ulaya aligundua anapenda sana ubunifu kuliko kitu kingine . na hapo ndipo alipo anzia kupenda kutayarisha muziki.
Mtu wa kwanza ktambulisha katika maswala ya muziki alikua mwanafunzi mwenzie Owen Shahada kutoka nchi ya Barbados ambaye alimfunza kucheza gitaa na kibodi.
Alirejea nyumbani mwaka wa 1996 na kufungua studio yake na kurekodi wimbo wake wa kwanza na bendi ya ‘the diplomats’.
Wakati Joseph Kosoga alipofungua kituo cha redio ilibidi Master J atafute njia mbadala ya kuwasilisha kazi zake kwenye jamii . Alijitahidi kuhamia mfumo wa digitali wa kurekodi.
Tazama highlights hapa:
Master J anayo shahada ya uhadisi wa umeme.Ubora wa kazi yake umedhihirika nchini kote kwa miaka miwili mfululizo, amepokea tuzo la muziki la Kilimanjaro Music Awards katika kipengele cha mtayarishaji bora wa mziki nchini. Nia yake ni kuwa bora zaidi na kuinua soko la mziki nchini Tanzania.
Ili kuona stori zingine nyingine kama hizi za kusisimua, tazama Maisha Yangu kila Jumanne saa 3:30 usiku ndani ya DStv 160 pekee!
