maisha magic bongo logo

Hukumu ya Elizabeth 'Lulu' Micheal

Habari14 Novemba 2017
Msanii maarufu Elizabeth 'Lulu' Micheal anapewa hukumu ya miaka miwili kwa kifo cha Marehemu Steven Kanumba.
LuluMicheal 1

Elizabeth Michael ‘Lulu’ muigizaji mashuhuri katika sanaa za televisheni amehukumiwa katika mahakama Kuu ya Tanzania kwa shtaka la mauaji bila ya kukusudia. Lulu alikuwa na mahusiano na msanii mwenzake mkongwe marehemu Steven Kanumba.

Inasemekana chanzo cha kifo chake kilikua jeraha alilopata kichwani. Inasemekana pia marehemu Steven Kanumba alisukumwa na Elizabeth Micheal, ambaye amehukumiwa miaka miwili gerezani kwa kusababisha kifo cha Steven kanumba aliyeaga dunia tarehe 7 Aprili 2012.

 Ndugu yake Kanumba ndiye aliyetoa ushaidi kortini na kueleza kwamba Lulu na Kanumba walizozana siku ambayo Kanumba alipata ajali na kufa. Alisema Lulu alitoka chumbani na kumweleza Kanumba amezirai. Repoti ya daktari, ilisema kwamba Kanumba alishaaga dunia kabla ya kufikishwa hospitalini.  Elizabeth alipelekwa moja kwa moja gerezani kutumikia hukumu yake.

Pata habari moto moto kila siku hapa Maisha Magic Bongo!