Logo
Jua Kali
channel logo dark

Jua Kali

160Tamthilia16

Hatari tatu za kutumia mitandao ya jamii kudeti – Jua Kali

Habari
03 Novemba 2023
Baada ya Naira kugundua kwamba alikuwa akiongea na Bwana Kaka tena itakuaje?
Jua Kali

Katika ulimwengu wa leo ni kawaida kwa watu kukutana na wapenzi wao au marafiki zao kutumia njia ya mitandao ya jamii, na Naira sio tofauti. Lakini kama vitu vingi mahusiano ya mitandaoni yana hatari zake pia. Soma hatari tatu zinazoweza kutokea ukiwa unatumia mitandao ya jamii kudeti.

  1. Uongo na Udanganyifu

Ukiwa unaongea na mtu ni rahisi kutoa taarifa za uongo kuhusu wewe wenyewe au wao kutoa taarifa ya uongo kwako. Wanaweza kubadilisha picha zao, kusema uongo kuhusu umri, elimu, au hata hali yao ya ndoa. Hii inaweza kusababisha watu kuingia katika mahusiano na mapenzi bila kujua ni nani anawasiliana naye kama vile yalivyomkuta Naira. Ni muhimu kuwa macho na kuchukua muda wa kumjua mtu vizuri kabla ya kujitosa kwenye mahusiano.

  1. Uvujaji wa Taarifa Binafsi

Kutumia mtandao kwa kudeti mara nyingi kunahusisha kutoa taarifa za kibinafsi kwa watu usiowajua vyema. Hii inaweza kuwa hatari kubwa, kwani taarifa hizo zinaweza kutumiwa vibaya au hata kusambazwa kwa watu wasiostahili. Kwa mfano, Naira alitoa taarifa za anapokaa bila kujua ni nani alikuwa anakuja kumchua kwake. Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa unadhibiti taarifa unazozitoa na kuhakikisha usalama wa taarifa zako binafsi.

  1. Ukosefu wa Usalama

Wakati mwingine, watu hukutana na wapenzi wao wa mtandaoni kwa mara ya kwanza katika mazingira yasiyo julikana. Baada ya kutumiwa gari, Naira alijikuta akipelekwa nyumbani kwa Bwana Kaka na kabahati nzuri tayari alishamjua. Kama angekuwa mtu asiye mjua angekua akijiweka hatarini wakati familia yake hawajui yupo wapi.

Jua Kali
Mitandao ya jamii kudeti - Jua Kali

Je umeshawahi kukutana na mtu kupitia mitandao ya jamii? 

Ndiyo84%
Hapana16%

Usikose kuangalia kipindi cha #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.