Juma na Siwema walikutana katika Maulid, Ilala. Juma alienda katika Maulid na mdogo wake aitwaye Ismail ambae ni rafiki wa karibu wa Siwema.
.
Katika kuangaza-angaza macho Juma akamuona mdogo wake akiongea na Siwema. Kufika nyumbani Juma hakusita kumuuliza mdogo wake kuhusu Siwema na kumuomba ampe namba yake ya simu, ila Siwema alimtaka Juma aiombe mwenyewe kama kweli kampenda kwa dhati.
Juma akajikuta anaongozana na mdogo wake akiwa anaenda kumtembelea Siwema. Mwishowe Juma akamtamkia Siwema yaliyomo moyoni na kisha kwenda kwa wazazi na kuwaambia kuwa anataka kumuoa Siwema.
Familia ya Juma ilikuwa na furaha sana kusikia Juma amepata mwanamke wa kiislamu, na familia ya Siwema ilikuwa na furaha ya kusikia kuwa amepata kijana mwema wa kumstiri binti yao.