Logo
channel logo dark

Mizani Ya Ushambenga

160Uhalisia13

Watu wa Nguvu- Mariam Wa Migomba na Dr.Kumbuka

Habari
19 Agosti 2019
mb_mchikicho_s10_e12_20190618_newadvice

 

Katika kipindi cha Mizani Ya Ushambenga, tuna majemedari wawili , Mariam Wa Migomba na Dr Kumbuka ambao kila Jumatano jioni, wanatuletea mzani ya mada mbali mbali, kutoka  majumbani, mitaani kwa lengo la kuhakikisha usawa .  Kwa kifupi tunawatambulisha kwenu vinara wa mambo haya ya kuwekwa sawa ,Bi Mariam wa migomba na Dr Kumbuka, kila Jumatano saa 1 Usiku kipindi #MIZANIYAUSHAMBENGA 

Dr KUMBUKA alizaliwa Dar es salaam, Tanzania.  Katika familia ya Watoto watatu yeye ni mtoto wa pili. Amesoma elimu yake ya msingi shule iitwayo kipawa iliyopo uwanja wa ndege, Dar Es salaam na akaendelea na masomo yake ya sekondari Kisaki sekondari Morogoro.

Baada ya hapo akajiunga na chuo cha Utumishi wa umma  Tanga. Na kupata diploma ya record.hakuishia hapo alisoma chuo cha sana ifakara na kuibuka kidedea shindano la mshehereshaji bora ktk shughuri mbali mbali za serikali na watu binafsi kama MC.

Pia alishinda shindano la mtaa kwa mtaa lilokuwa likifanywa na radio times fm nakuibuka kidedea na kupata kazi utangazaji ktk radio times fm iliyopo Dar Es salaam kawe beach kwenye kipindi cha mitikisiko ya pwani. Ndoto zake ni kuwa mshehereshaji Mkubwa ktk shughuri mbali mbali za kijamii na kuelimisha vijana na kumiliki kituo cha tv

MARIAM Wa MIGOMBA

Mariam Migomba alianza masomo yangu ya Msingi mwaka 1981 mpk 1987 shule ya Msingi Mgulani D'Salaam . Baadaye alijiunga na Masomo ya Secondary na kujiunga na chuo cha utangazaji TSJ Tanzania School Jounalism na kuhitimu na diploma mwaka wa 2003 .

Alipata  umaarufu Mkubwa mwaka 2012 ambapo kulikuwa na mashindano ya kumsaka malkia wa Taarab . Pale Mariam alishinda  Taji la Umalkia na mwaka 2014/2015 na pia kuwa Mtangazaji Bora nchini kupitia Radio Takriban 270. 

Mariam alibahatika kupata mafunzo kutoka BBC TRUST FUND na RFI Radio France Internatinal na akatunukiwa Cheti,na kutangazwa Balozi wa OMO. Na mwaka 2015 ailikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa vipindi Maisha Magic Bongo DSTVn na hadi Leo kipindi kinabadilika jina na kuitwa (Mizani ya Ushambenga). Kupitia hiki kipindi Mariam na Dr.Kumbuka kutoa Elimu na ushauri . Kwa hivi sasa Mariam ameamua kwenda kujiongezea Elimu ili afikie kuwa Mwanaharakati mzuri zaidi wa ushauri. 

                                        Kaa mkao wa kula sasa kila Jumatano saa 1 Usiku kipindi ni #MIZANIYAUSHAMBENGA ndani ya DStv160 pekee usikose.