Logo
channel logo dark

Mizani Ya Ushambenga

160Uhalisia13

Mtangazaji wetu Dr Kumbuka- Mizani ya Ushambenga

Habari
31 Oktoba 2019
Screenshot 2019-11-07 at 11.37.41

 

Dr Kumbuka  alizaliwa Dar es salaam, Tanzania.  Katika familia ya Watoto watatu na  yeye ni mtoto wa pili. Amesoma elimu yake ya msingi shule iitwayo kipawa iliyopo uwanja wa ndege, Dar Es salaam na akaendelea na masomo yake ya sekondari Kisaki sekondari Morogoro.

Baada ya hapo akajiunga na chuo cha Utumishi wa umma  Tanga. Na kupata diploma ya record.hakuishia hapo alisoma chuo cha sana ifakara na kuibuka kidedea shindano la mshehereshaji bora ktk shughuri mbali mbali za serikali na watu binafsi kama MC.

Pia alishinda shindano la mtaa kwa mtaa lilokuwa likifanywa na radio times fm nakuibuka kidedea na kupata kazi utangazaji ktk radio times fm iliyopo Dar Es salaam kawe beach kwenye kipindi cha mitikisiko ya pwani. Ndoto zake ni kuwa mshehereshaji Mkubwa ktk shughuri mbali mbali za kijamii na kuelimisha vijana na kumiliki kituo cha Tv. 

Usikose  Mizani ya Ushambenga kila Jumatano saa 1 Usiku