Logo

Burundani bila kikomo

Habari
03 Decemba 2019
mb_kapuni_s9_20191220

Wiki hii ni mwendo wa Burudani bila kikomo hapa MMBongo

Kwenye Rebeca Baada ya yale makasheshe ya wiki iliyopita, Sakina anazidi kudanganya huku nia yake haswa ikiwa haieleweki ni nini, Ussy bado anatapa tapaa.Wazazi wa Daniel wanabaki mdomo wazi baada ya kukuta mwanao kafanywa bwege.Simanzi linatawala nyumbani kwa kina Daniel, Albert katoka hosipitali na fahamu bado hazijarudi, je Caren atavumilia haya mbaka lini?  Kambona afika mahakami kwa ajili ya binti yake Rebeca.Kumbukumbu za Albert zimerudi, Daktari na Albert wote matatani, Je nini kitaendelea, Albert ameamua kuoa Doris! Caren atwaambia nini ? Usikose kuungana nasi.

Kwenye MadhubalaMambo ni bam bam! Maneno yametoka kwenye kinywa cha RK , Pengine haya ndiyo maneno tuliosubiri yanamtoke kinywani RK? Je Madhu atapokeaje haya ?  .Huku Mwamba RK mwenye mapenzi yake ya ajabu kwa mke wake anafanya uchunguzi . Dipali , Radha Bituji wote tumbo joto … ….Baada ya lile busu la ushindi  kigugumizi kinawashika wote wawili, anayo yasema Rk yanampanikisha Madhu,  je huu ni ule mwanzo tunaongojea kwa bashasha? 

Kwenye Huba , Devi anaonekana kufurahi na mwanae,Jude anajiroweka kwenye pombe Kibibi ofisini ni mwendo wa kupambana na mapacha , Roy anapropose ndoa kwa Nandy. Stano kambulia vibao kutoka kwa Tesa, Rani kakubali kushirikiana na Stano, Doris anazidi kumkomesha Roy, Tima katimua kila mtu.