Logo

Burudani ya Kipekee Juni Hii Ndani ya Maisha Magic Bongo!

Habari
01 Juni 2024
Tunasheherekea baba zetu Juni hii ndani ya Maisha Magic Bongo
Article

Jiya  – Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku

Jiya, mwanamke Mhindu anayetaka kuolewa kwa lazima, anaamini kuwa amependa kijana mweusi Don G, lakini hatima ina mipango mingine wakati anapokutana na kijana Masaai Senteu na mambo yanageuka kabisa.Baada ya kuachana na Don G na Sanjeet, Jiya akutana na Senteu na sasa hivi yupo kijijini na Jiya.

Kitimtim – Jumatatu na Jumanne saa 3 usiku

Ungana na Pili na familia yake ,hekaheka na maisha yao ya kila siku ni za kuvunja mbavu.Pili amamua kuachana na Zunde tena wakati Zunde akiendelea kudai mtoto.

Mpali – Jumatatu hadi Alhamisi saa 2jioni

Sakata la Nguzo na wake zake zaidi ya sita ,maisha yao ya kila siku ni ya visa , visanga , mashindano , wivu , usaliti , kila mmoja akijaribu kuitetea nafasi yake. Jiunge na msimu mpya wa Mpali.

Huba – Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku

Jiunge na msimu mpya wa Huba na gundua matukio yatakao yokea ndani ya familia ya Mzee JB na pia ona ni nini kimewarudisha Nicole na Devi.

Jua Kali – Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku

Baada ya Tony kurudi ndani ya Jua Kali, kazi yake imekuwa kuvuruga mahusiano ya Femi na pia mahusiano ya Maria.

Nuru (Msimu Mpya) - Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku

Tamthilia hii inahusu ndugu wawili waliochukiana wanajikuta lazima waungane kupambana na adui anaewatandia giza nene maishani mwao, baba yao.

Mizani ya Ushambenga – Jumamosi saa 2:30 usiku

Malkia wa huba na Blandina , wanatupa vionjo vipya na mada za kusisimua zinazo husu maisha yetu ya kila siku.

Dosari  – Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku

Dosari inafuatilia maisha ya Queen, mwanamke aliye katika kivuli cha himaya ya mumewe na anayetafuta kisiri kulipiza kisasi kutokana na utoto wa kufadhaisha. Katika kipindi hiki, tunamuona akijaribu kupata mahali pake na utambulisho wake, wakati bado anatafuta upendo wa chaguo lake mwenyewe.

 

Jiunganishe na #MyDStv App kwa burudani zaidi.