Logo
Screenshot 2022 09 20 at 12
channel logo dark

Yalaiti

160Drama16

Mastaa wa Afrika wajiunga na Maisha Magic Bongo!

Habari
07 Novemba 2022
Yalaiti na Jua Kali ya kuletea mastaa bingwa ndani ya bara la Afrika mwezi huu!
Untitled design (5)

Maisha Magic Bongo yazidi kupanda kimataifa kama baadhi ya chaneli bora ya televisheni ndani ya bara la Afrika. Kuanzia vipindi vyetu vya maongezi, miziki na pia tamthilia tumefanikiwa kuwaletea watanzania burudani ambazo ziwezakushindana na nchini zingine zilizoendea. Kwa sababu hii, hata waigizaji wa kimataifa wemejikuta wakiwa na upendeleo wa kuigiza ndani ya tamthilia zetu. Angalia orodha ya mastaa walioingia ndani ya tamthilia za Maisha Magic Bongo mwezi huu:

Sho Madjozi

Sho Madjozi ajulikana pia kwa jina lake la kuzaliwa la, Maya Wegerif. Ni mwanamuziki maarufu tokea Afrika Kusini. Sho Madjozi alijiunga na tamthilia ya Jua Kali akiigiza kama mwenyewe, mwanamuziki ambaye alikuwa akimsaidia Kitundu kwenye mashindano yake ya kucheza.

Van Vicker

Joseph Van Vicker anayejulikana kama Van Vicker ni muigizaji maarufu tokea Ghana. Van Vicker alishawahi kuigiza kama Bobo, mchumba wa Anna ndani ya #MMBJuaKali na mwezi huu arudui tena kama, Bobo, mpenzi wa zamani wa Anna. Baada ya Anna kwenda Afrika Kusini kwenye semina ya kazi ajikuta mikononi kwa Bobo tena na alazimishwa kuchagua kati ya Bobo na Diba.

Richard Mofe-Damijo

Richard Mofe-Damijo ni muigizaji kikongwe totea nchini Nigeria. Mwezi huu ajiunga na Jua Kali kama Professa aliyewafundisha Anna na Bobo, na anataka Anna na Bobo warudiane kimapenzi.

Celestine Gachihu

Celestine Gauchi ni muigizaji maarufu tokea Kenya, anajulikana sana ndani ya tamthilia ya Kenya, Selina, amabayo iliisha ndani ya chaneli ya Maisha Magic East mwezi wa Aprili mwaka huu. Kwa sasa, amejiunga na kipindi cha #MMBYalaiti kama, Diana.

Peter Kamau

Peter Kamau ni muigizaji maarufu tokea Kenya. Alishawahi kuigiza kama Biko ndani ya tamthilia ya Selina, iliyokuwa ndani ya Maisha Magic East. Mwezi uliopita talionekana kama mmoja wa waamuzi wa masindano ya kucheza, wakati Kitundu alivyokuwa Kenya. Mwisho wa mwezi huu anatarajia kujiunga na kipindi cha #MMBYalaiti.

Luthuli Dlamini

Luthuli Dlamini ni muigizaji tokea Afrika Kusini, aliyezaliwa nchini Zimbabwe. Luthuli ni kikongwe ndani ya tasnia ya filamu nchini Afrika Kusini. Mwezi huu ajiunga na tamthilia ya #MMBJuaKali kama bosi wa Kitundu, Bwana Bandili, baada ya Kitundu kuamua kuzamia Afrika Kusini.

Untitled design (5)
Mastaa wa Afrika ndani ya Maisha Magic Bongo

Je umefurahi kumuona nani ndani ya Maisha Magic Bongo?

Sho Madjozi14%
Celestine Gachuhi49%
Peter Kamau5%
Luthuli Dlamini5%
Richard More-Damijo8%
Van Vicker19%

Usikose kuburudika na tamthilia ya #MMBYalaiti kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku na  #MMBJuaKali kila Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.