Logo
Yalaiti HDtv 1920x1080

Yalaiti inaanza Julai – Maisha Magic Bongo

Habari
01 Julai 2022
Kipindi kipya cha Yalaiti kitaanza tarehe 4 July saa 4 usiku.
Yalaiti Showmax LandscapeHeroImage 1920x1080

Tunaanza mwezi huu wa Julai na tamthilia mpya ndani ya Maisha magic Bongo. Je maisha yalishawahi kukupiga mbaka ukaishia kusaema Yalaiti? Basi hauko peke yako.  Yalaiti ni tamthilia mpya inayohusu maisha katika jamii haswa kwenye mapenzi na ndoa.

Wapo wanawake au waume wenye kuithamini ndoa au mapenzi lakini wakapata wanawake au waume wasiothamini ndoa zao au mapenzi yao. Kuna pia wanawake wenye mali au nafasi lakini hawana bahati ya kuolewa na wakiolewa wanapata nuksi maishani. Kuna pia watu wanaoanza mahusiano vizuri lakini changamoto zikaingia mwisho wakawa maadui wakubwa. Ukiongeza marafiki waharibifu ndio mapenzi, mahusiano au ndoa zinasambaratika kabisa. Majuto ni mjukuu huja baadae. Yakikufika utasema YALAITI.

Usikose kuangalia kipindi cha #MMBYalaiti kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku ndani ya DStv chaneli 160!

Je upo tayari kuangalia hiki kipindi?

Yalaiti - Maisha Magic Bongo

Je upo tayari kuangalia hiki kipindi? - Tuambie

Ndiyo92%
Hapana8%
Kwa mengine zaidi: