Logo
Yalaiti HDtv 1920x1080

Wafahamu waigizaji wa Yalaiti! - Maisha Magic Movies

Habari
15 Julai 2022
Kipindi kipya cha Yailiti kinakuletea sura mpya na sura ulizowahi kuziona ndani ya Maisha Magic Bongo!
summer style (1)

Kutana na baadhi ya waigizaji wa #MMBYalaiti

Tanasha (Irene Paul)

Tanasha ana igizwa na Irene Paul, ambaye pia unaweza kumona ndani ya #MMBJuaKali. Tanasha anamiaka 35-40. Ni msomi na mchapa kazi na kazi yake ni supervisor wa Kilwa ICT. Tanasha bado hajaolewa na anaona umri unasongo na mapenzi yanamponza. Tanasha ni mkimya lakini ana akili nyingi.

Tika (Christopher Moris)

Tika ana umri taki ya miaka 25-30 na hana kazi kwa sasa.Anaishi maisha ya kutegemea wengine na ana hasira za karibu. Alikuwa akifanya kazi na Sacha na Rehema na alishawahi kuwa mpenzi wa Rehema secretary wa boss wake. Anamhadaa Tanasha kimapenzi kwa kuwa Tanasha anampenda

Sacha (Othman Njaidi)

Sacha ni kijana wa umri kati ya miaka 25-30, anapenda kuvaa vizuri na kupendeza. Anafanya kazi na Rehema na yeye na Tika wanapigania penzi la Tanasha. Rehema anajaribu kumtumia lakini hampendi na pia ni rafiki mkubwa wa Remmy

Zuwena (Ndumbagwe Misayo)

Zuwena ana umri wa miaka 30 na ni mke wa Hisan. Anafanya kazi Kilwa ICT chini ya Tanasha na ana mtoto mmoja mchanga. Hajielewi kimaisha na anatumiwa sana na Frida Zuwena afanya maamuzi kutegemea upepo unavyovuma. Anampenda mumewe lakini ulevi unamponza

Stella (Vanessa Mwalugala)

Stella ana umri wa miaka 25-30, ni mrembo na anayejua kuvaa. Alikuwa mchumba wa Remmy lakini hakuolewa na ana kisasi na Manka kwa kumchkulia mume. Aliwahi kuchepuka na Sokoine, baba mkubwa wa Remmy. Hamtaki Remmy lakini anataka kumtumia

Frida (Gysell Ngowi)

Frida ana miaka 30 na kivuruge. Ameolewa na Steve na ana watoto wawili. Anapenda sana anasa. Kama Zuwena ni bendera, basi Frida ndiye upepo. Anapenda sana kutoa maoni ya kutatanisha. Hampendi Manka na si mwaminifu katika ndoa.

Manka (Mwanahamisi Mziray)

Manka ana umri wa miaka 30 na ni mke wa Remmy. Ndoa yao ni changa yenye changamoto. Yeye na Stella ni mahasimu wa penzi la Remmy. Ana hasira na maamuzi ya haraka na anaithamini ndoa yake. Anawachukia marafiki wa Remmy na rafiki wake mkubwa ni Tanasha.

Remmy (Khizzer)

Remmy ana umri wa 30-35 na ni mtanashati. Anafanya kazi kwa kampuni tajika na ni mwana wa pekee wa wazazi wake. Ni mume wa ndoa wa Manka. Mahusiano yake ya awali na Stella yanavuruga ndoa yake. Ni mwaminifu lakini mkewe hampi amani.

Kilonzo (Omary Mohamed)

Kilonzo ana umri wa 25-30 ni kivuruge na rafiki yake na Remmy na Sacha. Anapenda sana starehe na ana hela kiasi cha haja. Anachepuka na mwanamke yeyote bila kijali kama mke wa mtu. Hajaona na hana nia ya kuoa ila kuponda Maisha.

Bichuka (Delitinus Deogratius)

Bichuka ana umri wa miaka 25-30, ni mpole na mwenye heshima. Ndiye anaye muasa Kilonzo, bado hajaoa lakini anasubiri mke mwema. Aliwahi kumtaka Zuwena awali. Wanajuana na Frida na ndio sababu Frida akampeleka Zuwena kwa Hisan. Na bado anampenda Zuwena ana atafanya lolote warudiane.

Usikose kuangalia #MMBYalaiti kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku na marudio ya wiki nzima Jumapili saa 5 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160!