Logo
Yalaiti HDtv 1920x1080

Stella au Manka? – Yalaiti

Habari
11 Agosti 2022
Msahidie Remmy kuchagua!
Screenshot 2022 08 11 at 09

Remmy amemuoa Manka, lakini kwa kulazimishwa. Baada ya wazazi wake kumkataza Remmy kumuoa Stella, alilazimishwa kumuoa Manka. Ingawa aliamua kumuoa Manka mawazo wake yote, bado yako kwa Stella.

Remmy alianza mapenzi na Stella wakati walivyokuwa kijijini, kabla ya kukutana na Manka. Wakati Remmy alivyofikia muda wa kuoa alimwabia baba yake kwamba alishapata mchumba na yupo tayari kumuoa. Wazazi wake walivyogundua kwamba ni Stella, walikasirika juu ya tabia ya Stella. Stella alishawahi kuwa na mahusiano na Rafiki yake na baba Remmy mpaka akabeba ujauzito wake. Baada yah apo alichukua pesa zake na kukimbia. Hili jambo lilimuonyesha Stella kama tapeli na wazazi wa Remmy hawakuweza kumona kama mtu mzuri na walimlazimisha kutafuta mke mwingine, na ndiyo hapo alipoamua kumuuoa Manka.

Kwa sasa ingawa Remmy yupo na Manka, bado mawazo yake bado yapo kwa Stella. Je aende na kinyume na wazazi wake na arudiane na Stella? Au aendelee na ndoa yake na Manka? Msaidie kuchagua hapo chini.

Screenshot 2022 08 11 at 09
Manka au Stella? - Yalaiti

Msaidie Remmy kuchagua hapo chini

Manka72%
Stella28%

Usikose kuendelea kuburudika na #MMBYalaiti kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku na marudio kila Jumapili saa 5 usiku kupitia DStv chaneli 160, Maisha Magic Bongo!