channel logo dark
channel logo dark

The Boy

160DramaPG13

‘Yolanda’ na ‘The Boy’ kuwasha moto ndani ya Maisha Magic Bongo Agosti hii!

Habari
01 Agosti 2024
Soma ratibi ya vipindi vya mwezi huu ndani ya DStv chaneli 160!
Article

The Boy – Jumatatu hadi Ijumaa 12 jioni

Fuatilia kipindi kipya cha Kituruki kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 12 jioni.

Yolanda – Jumatatu hadi Jumatano saa 1 usiku

Fuatilia maisha na shida zote za Yolanda kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1 usiku.

Jiya  – Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku

Jiya bado hajapatikana na Don G na Sanjeet wafanya kila kitu kumtafuta.

Kitimtim – Jumatatu na Jumanne saa 3 usiku

Ungana na Pili na familia yake ,hekaheka na maisha yao ya kila siku ni za kuvunja mbavu.Pili amamua kuachana na Zunde tena wakati Zunde akiendelea kudai mtoto.

Mpali – Jumatatu hadi Alhamisi saa 2jioni

Sakata la Nguzo na wake zake zaidi ya sita ,maisha yao ya kila siku ni ya visa , visanga , mashindano , wivu , usaliti , kila mmoja akijaribu kuitetea nafasi yake. Jiunge na msimu mpya wa Mpali.

Huba – Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku

Jiunge na msimu mpya wa Huba na gundua matukio yatakao yokea ndani ya familia ya Mzee JB na pia ona ni nini kimewarudisha Nicole na Devi.

Jua Kali – Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku

Baada ya Tony kurudi ndani ya Jua Kali, kazi yake imekuwa kuvuruga mahusiano ya Femi na pia mahusiano ya Maria.

Nuru (Msimu wa Mwisho) - Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku

Tamthilia hii inahusu ndugu wawili waliochukiana wanajikuta lazima waungane kupambana na adui anaewatandia giza nene maishani mwao, baba yao.

Kumi za Wiki – Ijumaa saa 11 jioni

Usikose kuangalia countdown ya ngoma zilizovuma ndani ya wiki.

Mizani ya Ushambenga – Jumamosi saa 2:30 usiku

Malkia wa huba na Blandina , wanatupa vionjo vipya na mada za kusisimua zinazo husu maisha yetu ya kila siku.

Dosari  – Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku

Dosari inafuatilia maisha ya Queen, mwanamke aliye katika kivuli cha himaya ya mumewe na anayetafuta kisiri kulipiza kisasi kutokana na utoto wa kufadhaisha. Katika kipindi hiki, tunamuona akijaribu kupata mahali pake na utambulisho wake, wakati bado anatafuta upendo wa chaguo lake mwenyewe.

 

Jiunganishe na #MyDStv App kwa burudani zaidi.