Logo
Slay Queen SP Billboard
channel logo dark

Slay Queen

160Drama16

Umeshakutana na Dk Chris toka Malawi?

Habari
11 Agosti 2020
Nana anazidi kuona ugumu wa kuwa na Chris wakati mama yake akiendelea kumchukia.
Kutana na Dr Chris Slay Queen


Msimu wa nne wa Slay Queen umeanza na kuonyesha mapenzi kati ya Nana na Chris yakiwa kwenye matata sana kwa sababu mama yake Nana alimkataa Chris kisa kuona kwamba ni mlala hoi asiyekuwa na pesa. Mama Nana anadai uzuri wake Nana haustahili kuwa na mtu wa hali ya chini, Nana bado hajitambui kwenye msimamao wake. Anampenda mama yake lakini pia anampenda sana Chris na hataki kuachana naye. Baada ya kufikiri sana ameamuwa kumuingiza Chris kwenye mchezo wa kumzunguka mama yake ili endelee kuwa na Chris. Aliamuwa kumleta Chris nyumbani na kumtambulisha kwa mama yake kama, Dr Chris!
Angalia utofati kati ya Dereva Chris na Dr Chris:
• ‘Dereva Chris' anatokea Dar es salaam, Tanzania wakati  Dk Chris anatokea Lilongwe,Malawi.
• ‘Dereva Chris' anafanya kazi kama dereva wa Dr Kileo wakati ‘Dk Chris' ni mwanafunzi wa udaktari.
• ‘Dereva Chris' hana familia ya karibu wakati ‘Dk Chris' anatokea kwenye familia ya utajiri sana.
• ‘Dereva Chris' anaongea lugha ya Kiswahili tuu, wakati ‘Dk Chris' anaongea kingereza na lugha nyingi zingine.
Kwenye karatasi Dr Chris ndio anayeoneka kama mwanume bora kwa mama yake Nana, lakini kama nana alivyosema amekutana na wanaume wengi kama Dr Chris lakini hawaku mueshimu hau kumpenda saa hii kama dereva Chris alivyo mpenda, je unadhani  Nana ana haki ya kumpenda yeyote anaye taka au ni lazima amsikilize mama yake?


Usikose kuangalia kipindi cha Slay Queen kila Jumatano mpaka Ijumaa saa 3:30 usiku na marudio kila Jumamosi kuanzia saa 8 mchana, ndani ya Maisha Magic Bongo chaneli 160 pekee.