Kisima cha burudani ndivyo tunavyojulikana, na nia yetu siku zote daima ni kukuletea burudani bila kikomo kila siku. Kwa wadhifa tulionao sisi Maisha Magic Bongo, yetu ni wewe mtazamaji wetu ufurahie uelimike na kupata burudani za aina mbali mbali kia siku. Hivyo basi mwezi MEI 2020 tuna furaha na bashasha kabisa kuwaletea Tamthilia ya kukata na shoka ‘’SLAY QUEEN’’.
Maudhui ya tamthilia hii sio kitu kigeni katika macho yetu, Maisha yetu, na jamii zetu kwa ujumla. Kwani Familia hii iliyopambana sana kujitoa katika umsakini wanafanikiwa na kuwekeza katika kampuni kubwa ya mawasiliano , na kama tunavyojua mafanikio na utajiri yanakujaga na mengi sana, kwani Mzee Kasongo maarafu kama JB , mmiliki wa kampuni hiyo pesa zinampanda kichwani anavuruga familia na kutumbukia kwenye dimbi la mapenzi na maSlay queen, kwa kifupi anajisahau kabisa na hapo ndipo drama zinapo anzia.
Watoto wake Derick na Juliet maarufu kama TESS CHOCLATE, wanapitishwa katika majaribu makubwa na baba yao.Tamthilia hii ni ya tofauti na imejaa wasanii wakongwe kama vile Richie Richie na wengine wengi .
Ungana nasi, tarehe 6 Mei 2020, uwe wakwanza kuhadithia tamthilia ya SLAY QUEEN kupitia channeli yako pendwa, ni Maisha Magic Bongo, DSTv chaneli 160 #NIYetu