Logo
Slay Queen SP Billboard
channel logo dark

Slay Queen

160Drama16

Michezo ya Mami – Slay Queen

Habari
12 Novemba 2020
Mami amemuweza Derrick na kumuacha hoi baada ya kuolewa naye harafu kuchukuapesa zake zote na kutoroka Tanzania
Mami Slay Queen

Tangu kulivyokutana na Mami, alikuwa ni dada liye jielewa sana. Mwanzoni alionyesha kwamba alimpenda Derrick sana. Lakini, baada ya muda unaweza kuanza kujiuliza, je ni kweli alimpenda Derrick au aliona Derrick kama mtoto wa tajiri anayeweza kumpa maisha bora?

Maswali haya yote yanakuja baada ya Mami kuendelea kumng’ang’ania Derrick ingawa muda wote Derrick alikuwa na Agnes na alimwambia Mami kwamba anampango wa kumuoa Agnes. Mami alikasirika lakini akaendelea kukutana na Derrick mpaka usiku wa harusi yake.                                 

Alivyofumwa, na Agnes alivyo msamehe, alirudi kumwambia Mami hamtaki na Mami akapata mchumba mpya. Lakini baada ya kusia kwamba Agnes alimsamehe Derrick na walikuwa mpango wa kufunga ndoa tena.Mami alirudi kwa Derrick kudai msamaha kwenye siku yake ya harusi. Agnes alivyowafuma tena, alikasirika na kumuacha Derrick kabisa. Mami alitumia muda huo kumwambia Derrick amuoe yeye walivyokuwa wamelewa. Derrick alivyo muoa tuu, Mami alichukua pesa zake zote na kwenda Ulaya.                                                                                                                                                       

Derrick anamishe sasa za kumtafuta Mami, je atapata pesa zake? Usikose haya yote ndani ya#SlayQueenTZ kila Jumatano hadi Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.