Agnes na Derrick najiandaa kufunga ndoa tena kwa mara ya pili baada ya mikosi iliowakuta mara ya kwanza. Balaa lao halikuanzia kwenye ndoa tuu, lili anzia kwenye siku yao ya kuvishwa pete. Kabla ya Derrick kumvisha pete Agnes, Alice alitokea na kudai kwamba yeye anampenda Derrick zaidi na Derrick amuoe yeye.
Baada ya hiyo kasheshe, walifanikiwa na kuendelea na engagement na kufanya mipango ya kufunga ndoa. Lakini siku ya harusi, Derrick alipotea, na kufumwa ndani ya nyumbani kwa Mami. Agnes alikasirika sana na kuamuwa kuacha na Derrick.
Baada ya kifo cha mama yake Derrick, Agnes na Derrick waliamu kurudiana. Agnes akamuwa kumpa Derrick mashariti kwenye mahuasiano yao na baada ya muda wakanza kupanga harusi yao tena. Lakini kwa jinsi mikosi ilikuwa ndani ya mahusiano yao bado Agnes na familia yakewana wasiwasi na harusi hii. Usikose kuangalia Slay Queen Tanzania kila Jumatano mpaka Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya chaneli 160, Maisha Magic Bongo.